Watoto wa mtaani wanaojishughulisha na shughuli za kujipatia kipato katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi, eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam, wakiwa wameuchapa usingizi huku mmoja wao wakijiuliza na kujishauri kuamka wakati baadhi yao tayari wakiwa wameamka na kuanza kazi za kusafisha Vioo vya magari eneo hilo latika foleni ili kujipatia chochote kwa ajili ya kununua chakula.
Hawa ni baadhi yao wakiwa tayari wameamka wakipeana vifaa vya kufanyia kazi ili kuanza kazi yao ya kuosha vioo vya magari.
Kwa uchunguzi ulifanywa na blog yako ya jamii millionfortune hot news, tumegundua wimbi la kuongezeka kwa watoto hawa wa mitaani linatokana na kupungua kwa malezi sahihi katika jamii na baadhi ya wazazi kutohudumia vema familia zao au kukwepa majukumu hivyo watoto wengi kuachwa wakiishi na bibi au babu zao ambao wengi wamekuwa hawawezi kuwalea wajukuu zao vema. Aidha kwa kutumia mwanya huo watoto hao wamekuwa wakitoroka na kuja mijini kutafuta maisha na huishia kuwa watoto wa mitaani na wengi wao huishia kutumia madawa ya kulevya, bangi na miraa na kazi zao kubwa kupora na kuiba vitu huku wakijishikilia chini ya miamvuli ya kazi kama kuosha vioo vya magari katika mataa na kubeba mizigo.
ANGALIZO:
TAIFA LA KESHO LINAELEKEA WAPI ? WATOTO HAWA WENGINE WANAKUA NA KUWA WATU WAZIMA WAKIWA KATIKA HALI HII NA MAZINGIRA HAYA MWISHO WAKE NI NINI?
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!