Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Pichani ni wananchi waliokataa kuhesabiwa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Bwana Guram Hussein Kifu. katikati ni Kiongozi wa Mgomo Bwana Ally Mwangoto, kutoka dini ya Kiislamu wanaojiita wenye msimamo mkali wakiwa chini ya ulinzi katika mahabusu ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Ruiwa,Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya,wakisubiri kupelekwa Polisi wilayani humo.
Licha ya Rais Jakaya Kikwete kuwataka waislamu nchini kushiriki zoezi la Sensa ya watu makazi, hali hiyo imeonekana kuwa tatizo kwa kijiji cha Ruiwa Kata ya Ruiwa Wilayani Mbarali ambapo watu wasita wanaosadikiwa kuwa ni waislamu wenye msimamo mkali kugoma kuhesabiwa kwa madai kuwa serikali imepuuza madai yao.
Imeelezwa kuwa waislamu hao walishaeleza serikali kuwa hawako tayari kuhesabiswa lakini bado serikali imeshindwa kutekeleza matakwa yao na hivyo kukataa kuhesabiwa.
Akizungumza na BLOG YETU jana kuhusiana na madai hayo, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ruiwa Bw. Jordan Masweve alisema kuwa kwa kata zoezi la sense toka limeanza imekuwa ni tatizo kubwa sana kutokana na watu hao kuonyesha msimamo wao wa kutotaka kuhesabiwa.
“Wao wanadai kuwa hawapo tayari kuhesabiwa hata iweje msimamo wao ni mmoja hata wafanywe nini lakini suala ni kutokubali kuhesabiwa tu kwa madai serikali imeepuza madai yao toka mwanzo ya kutotaka kuhesabiwa”alisema.
August 31, 2012
WALIOIGOMEA SENSA WAKIONA CHA MTEMAKUNI, HEBU FUATANA NAMI HAPA!
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!