Wananachi wa Mwangata Iringa wakishuhudia ajali hiyo asubuhi ya leo
Gari la TANESCO Iringa likitoa msaada wa lori lililopinduka usiku wa leo eneo la Mwangata Iringa
Watu kadhaa wamenusurika kifo usiku wa kuamkia leo katika eneo la Mwangata katika Manispaa ya Iringa baada ya lori walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka .Ajali hiyo mbaya imetokea eneo la kona ya Mwangata ambapo inadaiwa kuwa dereva wa lori hilo ambalo lilikuwa limebeba kokoto kuendesha lori hilo bila kuzingatia sheria za usalama barabarani na kutaka kukata kona huku akiwa na spidi zaidi ya 100 hali iliyopelekea lori hilo kuacha njia na kupinduka.
Mashuhuda wa tukio hilo wameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com baada ya kufika eneo la tukio na kushuhudia zoezi la kuliinua lori hilo likifanywa kwa msaada wa lori ya winchi la shirika la umeme nchini (Tanesco ) mkoa wa Iringa.
Hata hivyo walisema mbali ya abiria waliokuwemo katika lori hilo kunusurika kifo pia wakazi wa nyumba moja iliyopo jirani na barabara eneo hilo pia wamenusurika kutokana na lori hilo kutaka kugonga ukuta wa nyumba hiyo na iwapo lisingepinduka basi lingeweza kuvunja ukuta na kuingia moja kwa moja katika nyumba hiyo .
Katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha na dereva wa lori hilo anadaiwa kukimbia baada ya ajali .
Na Francis Godwin - Iringa
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!