Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Baadhi ya Madiwani na Masheha wa Shehia mbali mbali za Pemba, wakiwa katika Semina ya siku tatu Kuhusu Uimarishaji uhusiano baina ya Viongozi wa Kisiasa na Kiutendaji katika Serikali za Mitaa, iliyoanza chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, katika Ukumbi Misali Sunset Beach Hotel Wesha Pemba. Picha na Ramadhan Othman, Ikulu]
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
VIONGOZI wa Serikali za Mitaa wakiwemo Masheha wametakiwa kutojihusisha na migogoro ya ardhi kwani inaathiri maendeleo ya kilimo, utalii na makaazi ya watu na wakati mwengine huathiri hata amani na usalama katika maeneo yao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein aliyasema hayo leo katika ufunguzi wa semina ya siku tatu ya Viongozi wa Serikali za Mitaa, inayofanyika katika hoteli ya Misali, iliyopo Wesha Pemba. Katika hotuba yake kwenye ufunguzi wa semina hiyo, Dk. Shein alisema kuwa ni bahati mbaya kwamba mara nyingi Masheha na viongozi wengine wa Serikali za Mitaa ikiwemo Wizara husika, huwa wanajihushisha na migogoro hiyo.
Alisema kuwa kwa hakika migogoro hii inavuruga ustawi wa uchumi pia, kutokana na ukosefu wa maadili pamoja na kutokuzingatia sheria ziliopo kwa baadhi ya watendaji matokeo yake ni kuwanyima haki zao wananchi wanaostahiki na kupelekea kunungunika.
“Katika yatakayozungumzwa hapa ni suala la ardhi, jambo lenye kuleta utata na migogoro katika jamii Unguja na Pemba na pia ijulikane kuwa tatizo hili si la Zanzibar pekee bali ni la nchi nyingi duniani”,alisisitiza Dk. Shein.
Aidha, Dk. Shein alieleza kuwa katika mfumo wa utawala wan chi, viongozi wa Serikali za Mitaa wakiwemo Masheha na Madiwani wana jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba misihgi ya utawala bora inatekelezwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akiendesha Semina ya siku tatu ya Mashehe na Madiwani wa Shehia za Pemba katika ukumbi wa Misali Sunset Beach Hotel Wesha Pemba, (kulia) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, (kushoto) Waziri wa nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyihaji Makame na katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee. [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]
“Kama nilivyosema kule Unguja, nyie hapa ndio mlioko mashinani na mti wenye shina bovu hauwezi kusimama. Kwa kuzingatia haya, tumeamua kuendesha semina hii maalum kwenu ili kukupeni na nyinyi maelekezo na fursa kamili katika kujadili utawala bora,” alisema Dk. Shein.
Dk Shein alisema kuwa Utawala Bora ni kiini cha ustawi wan chi, amani na utulivu wake na kusisitiza kuwa malengo yote ya nchi yakiwemo uchumi na huduma za jamii yanalenga katika kuleta Utawala Bora kwa wananchi.
Kutokana na hali hiyo, Dk. Shein alieleza kuwa katika awamu ya Saba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa, suala la utawala bora lina umuhimu wa pekee. Pia, alitoa shukuran kwa UNDP kwa kufankisha semina hiyo. Pia, kwa upande wa Masheha na Madiwani wametakiwa kuwa na mashirikiano na uhusiano mkubwa katika kutunza amani na usalama ndani ya shehia zao.
Aidha wameelezwa kuwa ulinzi unaotolewa na vyombo vya dola au Polisi Jamii ambao unawapa usalama wananchi utafanikiwa tu kwa mashirikiano yao na wahusika wengine. Viongozi hao pia, wametakiwa lazima watambue kwamba utekelezaji wa mipango ya maendeleo unaofanywa na Serikali kwa kupitia kwenye Idara na Wizara zake huwa unatekelezwa katika shehia, zikiwemo upelekaji huduma za afya, elimu, maji na nyenginezo.
September 27, 2012
DKT SHEIN AWAASA MASHEHE WASIJIHUSISHE NA MIGOGORO YA ARDHI
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!