StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 27, 2012

RAIS JK ATOA RAMBIRAMBI KIFO CHA JENERALI ANATORY KAMAZIMA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Brigedia Jenerali Mstaafu Tindamanyire, ndugu wa hayati Meja Jenerali Mstaafu Anatoli Kamazima, nyumbani kwa marehemu Tegeta, Dar es Salaam. Kulia kwa Rais ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na Mnadhimu Mkuu Luteni Jenerali Samwel Albert Ndomba. Marehemu Kamazima, ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia Jumatano Septemba 26, 2012 utokana na mshtuko wa moyo, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU.


RAIS Jakaya Kikwete amemtumia salamu za pole Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kufuatia kifo cha Meja Jenerali Anatory Ruta Kamazima (Mstaafu) aliyefariki Septemba 25, 2012 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

“Nimepokea kwa mshituko na huzuni nyingi habari za kifo cha Meja Jenerali Kamazima, ni pigo kubwa sana kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Taifa kwa ujumla” Rais amesema katika salamu hizo.



Marehemu Meja Jenerali Kamazima
Mchana wa leo Rais ameitembelea familia ya marehemu nyumbani kwao Tegeta kuwafariji wafiwa.
Marehemu alizaliwa mwaka 1946 katika kijiji cha Maruku, Mkoani Kagera. Alijiunga na Jeshi mwaka 1967, mara baada ya kuhitimu Chuo Kikuu mwaka 1966.

Marehemu Kamazima amesoma kozi mbalimbali za kijeshi hapa nchini na nchi za China, India, Uingereza na Misri na kulitumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika ngazi mbalimbali ambapo mwaka 1989, aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Kuzuia Rushwa Tanzania, hadi alipostaafu Juni 2003. Rais amemuelezea marehemu Kamazima kama mzalendo na mtu aliyeipenda na kuitumikia nchi yake kwa weledi mkubwa, uaminifu na moyo mmoja.

“Nimemfahamu Marehemu kwa miaka yote ya utumishi wake jeshini na serikalini kama mzalendo, muaminifu na mwenye moyo wa kulinda nchi yake wakati wote” amesema “Marehemu Kamazima alikua mtu wa kutumainiwa sana katika nchi yetu na kamwe hatutamsahau kwa utumishi wake uliotukuka”.

“Tutamkumbuka na kumuenzi siku zote, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote na tunamuombea mapumziko mema Marehemu Kamazima. Amina”. Rais ameongeza.
Marehemu ameacha mjane, watoto na wajukuu.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat