Wajameni eeh huo ndo usafiri huku vijijini kwetu. Picha hizo zipigwa jana katika moja ya barabara iendayo Korogwe vijijini.Basi hilo lililopakia abiria wengi mpaka wengine kuwekwa katika keria ambapo kwa kawaida sehemu hiyo huwekwa mizigo jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao, lilikuwa likitokea Korogwe Mjini kuelekea Kata ya Magamba kwalukonge (Korogwe vijijini) Umbali wa takribani Km 109 kutoka Korogwe Mjini.
Najua hali ngumu tunatafuta hela (kwa upande wa wanaomiliki gari) na pia najua gari ndo hilo moja na pengine tutachelewa katika mihangaiko yetu ya kutafuta hela(kwa upande wa abiria), ila jamanii binafsi yangu nimejiuliza, vipi kuhusu usalama? Wahenga walisemaaa haraka haraka haina baraka....unaweza kuwahi katika hali hatarishi na usifike...jamani watanzania wenzangu kweli sasa nimeamini sikio la kufa halisikii dawa
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!