StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 18, 2012

MCDONALD LIVE MVOMERO YATEMBELEWA NA WAHANDISI KUTOKA NCHI 18 AFRIKA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Mkufunzi wa Live Line wa Kampuni ya McDonald Live Line Technology Ltd Donald Mwakamele (kulia), akitoa maelezo kuhusu vifaa mbalimbali vinavyohusu umeme kwa baadhi ya wahandisi 18 kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliofanya ziara ya mafunzo katika Kituo cha Mafunzo cha McDonald Live Line kilichopo Dakawa Wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro hivi karibuni ili kujionea kwa vitendo jinsi teknolojia ya ukarabati wa miundombinu ya umeme bila ya kukata nishati hiyo, ijulikanayo kama 'Liveline', inavyofanya kazi.

Wahandisi hao ambao walikuwa wakihudhuria mkutano mkubwa wa Sekta ya Umeme Afrika Mashariki (EAPIC), uliofanyika jijini Dar es Salaam Septemba 10-13, na kuwakutanisha watendaji wakuu wa makampuni 26 kutoka nchi mbalimbali zinazojihusisha na nishati ya umeme katika bara la Afrika.

CHINI: Ni mtiririko wa matukio mbalimbali ya ziara ya mafunzo ya wahandisi hao. PICHA ZOTE/DAILY MITIKASI BLOG













Kikosi kazi cha Wanahabari walioambatana na Wahandisi hao Mkoani Morogoro: (Kutoka kulia) ni John Badi (IPP Media & Daily Mitikasi Blog), Harriet Makweta (Mwananchi), Job (Jambo Leo), Khadija Kalili (Tanzania Daima & Bongo Weekend Blog), Jerome Risasi (Clouds TV & Radio), Kambi (Mtanzania), Peter Shadrack (Channel Ten) na Bashir Nkoromo (Uhuru & Daily Nkoromo Blog), katika picha ya pamoja nje ya Hoteli ya Nashera mkoani Morogoro muda mfupi kabla ya kuanza safari ya Mvomero.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat