Usizame inafuraha kuwatangazia kuwa mitambo yake ya ufumbuzi ya kutumia ujumbe mfupi wa SMS za bure kwa wasafiri wanaotumia vyombo vya usafiri vya baharini Tanzania vipo tayari kwa majaribio.
Kikosi cha Usizame kitafanya majaribio ya mitambo yake iliotengezwa kwa ufundi mkubwa na wataalamu wakujitolea wanaotumia maandishi maalum ambayo ambayo yataweza kuchanganywa na ujumbe mfupi wa SMS. Na baadae mitambo hiyo itafanya maribio yak echini ya kiwango kidogo katika hatua za awalai na majaribio hayo yatakuwa baina ya Unguja, Pemba na Dar es Salaam.
Umuhimu wa kuwajuvya watu kwa kupitia vipeperushi na kupitia kwenye vyombo vyengine vya habari kama vile redio na TV, hali kadhalika tutawashuru wale wote watakaotoa msaada wao katika kuwafikishia watu ujumbe huu.
Mpango huu umesarifiwa kwa ajili ya kukuza usalama wa abiria baada ya ajali mbili mbaya za baharini uliotokea chini ya mwaka mmoja, ajali ambazo zimepelekea vifo vya watu wengi. Mpangilio wa utaratibu huu utawezesha kuweka vifaa kwenye vyombo vya baharini ambavyo vitapelekea abiria kwa umoja wao kuhakikisha chombo wanachosafiria kipo tayari kwa safari za baharini.
Picha za majaribio kwa toleo hili zipo tayari kwenye database ya Usizame.
Usizame pia imekwisha maliza kazi ya kusarifu mtandao wake na tayari kwa matumizi kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea mtandao ili kuona vipi mitambo hiyo ifanyavyo kazi, na pia kujua kazi zilizofanyika katika mradi huu.
Kwa sasa mitambo hii inaweza kutumia ujumbe mfupi wa maandishi wa SMS utakaoweza kuandikisha abiria watakaokuwa wanasafiri na pia kuweza kuwajuulisha wenyewe kuwa wamesajiliwa kama wasafiri kwa wakati huo. Mara tu hatua nyengine ya mitambo hii itakapokamilika, taarifa zitatolewa kwa jamii nzima kwa ujumla.
Hivyo tunawasisitiza watu wote kufikisha ujumbe huu kwa jamii nzima, na kila atakaeona ama kusoma matangazo haya kuwaarifu wenzao, marafiki, ndugu, wafanyakzi wenzako, mawakala wa usafiri, waendeshaji wa vituo vya utalii na nyumba za wageni. Vile vile tunawaomba wote kujiandikisha kwenye mtandao wetu ili kuweza kupokea taarifa zote kwa wakati Usizame ipo hewani. Na tuifanye bahari ni sehemu ya usalama ya usafiri.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!