StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 20, 2012

MKUTANO MKUU WA BARAZA LA USALAMA BARABARANI WAFANYIKA MKOANI IRINGA LEO.

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mohamed Mpinga akizungumza mambo mbalimbali mapema leo mchana kwenye mkutano Mkuu wa Baraza la usalama Barabarani mkoani Iringa uliofanyika ndani ya ukumbi wa chuo kikuu cha Ruaha (RUCO),ambapo pia mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo hali ya usalama barabarani nchini,Sera ya Taifa ya usalama barabarani,Taarifa ya ukaguzi wa utendaji wa kikosi cha usalama barabarani katika kusimamia sheria na ukomo wa mwendokasi wa magari,Rushwa na Miundombinu ya uadirifu na mengineyo.Mkutano huo umefanyika wakati wiki ya usalama barabara ikielekea ukingoni.

Sehemu ya Takwimu za ajali barabarani.

Pichani juu na chini ni baadhi ya Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Baraza la usalama Barabarani mkoani Iringa wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa mapema leo ndani ya ukumbi wa chuo kikuu cha Ruaha (RUCO).

Mkurugenzi wa Udhibiti na usafiri wa barabara SUMATRA,Bwa.Aron Kisaka akifafanua jambo mapema leo mbele ya Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani nchini kwenye mkutano mkuu wa Baraza la Taifa la Uslama Barabarani uliofanyika ndani ya chuo cha RUCO,Mkoani Iringa.

Baadhi ya Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Baraza la usalama Barabarani mkoani Iringa wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa mapema leo ndani ya ukumbi wa chuo cha RUCO.

Sehemu ya Meza kuu ya Mkutano wa Baraza la Taifa la usalama barabaranii wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.

Pichani juu na chini ni baadhi ya Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Baraza la usalama Barabarani mkoani Iringa wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa mapema leo ndani ya ukumbi wa chuoha kikuu c cha RUCO.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat