Kimaadili, sitetei alichokifanya, ila kisheria ni sawa kwa mtu kwenda jela kwa kufanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha nne? Sijui kama umri umebadilika siku hizi lakini tulipokua kidato cha nne, mimi na wanafunzi wenzangu wote tulikua na umri kati ya miaka kati ya 16 na 18. Ingawa tulikua wanafunzi, tayari tulikua watu wazima na tulijua mabaya na mazuri, na tulijua tunachokifanya. Nilivyodhani mimi, sheria kama hizi ni za kuwalinda wasichana/wavulana wenye umri mdogo ambao hawajapevuka kiakili; lakini kwa mtu aliyekua kidato cha nne, akipata mimba ni uzembe wake maana ana umri wa kutosha kujua anachokifanya. Na sidhani kama kazi ya sheria ni kulinda uzembe wa watu. Au mnaonaje? Na kama mwl. Lukindo anakwenda jela kwa miaka mitatu, je huyo msichana naye ataadhibiwa maana na yeye alishiriki katika tendo hilo na ana umri wa kutosha kutambua athari za anachokifanya?
Anyway, back to the story, akisoma mashtaka katika shauri hilo, Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Elibaliki Polanjo, aliiambia mahakama kuwa kati ya Novemba mwaka jana na Februari mwaka huu katika Kijiji cha Magamba, mwalimu huyo, wa shule ya msingi ya Magamba iliyopo Handeni, Tanga, alikuwa akifanya mapenzi na mwanafunzi huyo na baadaye, kumpa ujauzito.
Katika kesi hiyo iliyokuwa chini ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Handeni, Patrick Maligana, mshtakiwa alikiri kosa lake, akikubaliana na maelezo yote yaliotolewa na mwendesha mashtaka.
Kufuatia hatua hiyo, Hakimu Maligana, alimtia hatiani na kumhukumu kutumikia adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.
Akifafanua kuhusu adhabu hiyo, Maligana alisema mshtakiwa alitenda kosa baya na hasa ikizingatiwa kwamba ni mwalimu anayepaswa kuwa mfano mzuri katika jamii, kwa kuzuia na kukomesha wimbi la matukio ya wanafunzi wa kike kupata mimba.
“Sheria inasema mwanaume yeyote atakayempa mimba mwanafunzi atakuwa ametenda kosa na kama atapatikana na hatia, atastahili kutumikia kifungo kisichopungua miaka mitatu jela na kisichozidi miaka sita. Kwa hiyo sheria hiyo inalinda wasichana kutokana na status yao, ya kama ni wanafunzi au la, na sio kutokana na umri wa kuelewa/kutoelewa athari ya kinadhofanyika? Ina maana ni sawa kufanya mapenzi na msichana wa miaka 14 asiyekuwa mwanafunzi lakini ni kosa kufanya mapenzi na msichana wa miaka 18 aliyekua mwanafunzi? Naomba mnielimishe mnaoelewa sheria hii maana kwangu it doesn’t make sense at all)
Kwa Kosa hili halitakuwa na nafasi ya kulipa faini,” alisema Maligana. Aliongeza kuwa adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa walimu na wanaume wengine wenye tabia ya kupenda kufanya mapenzi na wanafunzi wa kike. (Vipi kuhusu mwalimu wa kike akifanya ngono na mwanafunzi wa kiume enh? Sheria hapo inasemaje? Hmm?)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!