StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 25, 2012

AUSTRALIA YAHARAKISHA KUUKARIBISHA UCHUMI UNAOFUATA SHERIA ZA KIISLAM

Tweeted this Like this, be the first of your Friends




Serikali ya Australia itapeleka kundi la wataalamu nchini Dubai kwa ajili ya kujadili njia za kuendeleza uchumi unaofuata sheria za kiIslam nchini Australia. Ujumbe huo utakaongozwa na mtaalamu wa kiuchumi wa Australia ndugu Barry O’Farrell na wataalamu wengine wa mambo ya kiuchumi, watajadili maswala mazima yanayohusiana na usimamizi na sheria za uchumi huo, wakati huohuo ujumbe huo utatembelea mji wa Abu Dhabi na Lebanon.
Australia ina mategemeo ya kua na mchango mkubwa ktk uchumi huo kwa kuzingatia kwamba nchi za kusini mashariki mwa Asia ambazo zina uhusiano wa karibu na nchi hiyo, uchumi unaofuata sheria za kiIslam unakua kwa kasi. Moja ktk matatizo yaliyopo ni pamoja na uhakika kwamba juhudi za kupitisha sheria ya kuuruhusu uchumi huo kasi yake ni ndogo sana ktk ngazi za juu, kitu ambacho kimeilazimisha serikali ya Australia kuingilia kati. Serikali ya Austaralia ina hamu kubwa ya kujihusisha na uchumi huo alisema Salim Farrar muhadhiri mkuu wa kitengo cha sheria ktk chuo kikuu cha Sydney ambae alikiri vilevile kwamba swala hilo linahitaji mtiririko wa majadiliano ya kisiasa. Pamoja na mambo mengine Australia inakabiliana na changamoto zinazohusiana na sheria mpya za uchumi unaofuata sheria za kiislam hususan ktk maswala mazima ya Islamic bonds na triple tax duties. Kwa maelezo zaidi wasiliana na http://ijuebankyakiislam.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat