StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 18, 2012

NOTI MPYA ZATUMIKA KUTENGENEZEA POMBE NA KUVUTIA SIGARA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends  
BAADA ya kuzuka mtindo wa kuzikataa Sarafu za Shilingi 10 na Shilingi 20 kutotumika huku Benki kuu ikikaa kimywa, baadhi ya wananchi wameanza kuziharibu kwa makusudi noti za shilingi 500 na 2000 kwa kuondoa mstari(ufito) unaong'aa na unaohalalisha pesa hizo na kisha kuutumia katika pombe za kienyeji au bia ili kuongeza kileo wakidai kuwa husaidia kuokoa pesa kwani hulewa kwa muda mfupi.


Wananchi hao pia wanachomoa ufito huo na kuchanganya na sigara au tumbaku ambapo hudai hulewa haraka.

Hali hiyo ambayo imeambatana na uadimikaji wa noti hizo, imeshika kasi maeneo mengi nchini likiwemo eneo la Kijiji cha Maleza,Kata ya Kipeta,Wilaya ya Sumbawanga Vijijini.


Athari hiyo pia imevikumba vijiji vya Kilangawana na Kamsamba hali ambayo imefanya kuwepo kwa ugumu wa upatikanaji wa fedha hizo.


Hata hivyo wananchi kadhaa ambao hawakupenda majina yao kutajwa,wamethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kuitaka Serikali na Benki Kuu kuchukua hatua za haraka ili kukomesha vitendo hivyo.


Katika hali ya kuhalalisha noti hizo zilizoharibiwa wahalifu hao hutumia gundi kwa kutumia uzi wa mifuko ya mbolea ili ziendelee kutumika.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat