Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
HAPA NI MANZESE!
Mfano halisi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi inayoendelea kujengwa kwenye barabara ya Morogoro, katikati ni sehemu ya kituo cha abiria na mabasi ya kasi, pembeni ni barabara ya magari ya kawaida.
Pichani hapo juu unaonyesha mfumo huo utakavyokuwa kwenye eneo la Manzese. Mamlaka inayohusika na usimamizi wa Ujenzi huo ya DARTS wamekua wakitoa maelezo kwa muda mrefu hassa kwenye maonyesho mbalimbali yanapofanuika lakini si aghalabu watu wote kuweza kufika.
Kwa mamtiki hiyo ningependa ndugu wasomaji muelewe yakuwa mfumo huo unaonekana pichani ndiyo mfumo wenyewe utakavyokuwa, kwamaana kinachoonekana katikati ni kituo ambacho kisingi kitawahifadhi abiria wote wanaokwenda na kurudi mjini (Kariakoo, Posta na Fery) na mabasi yaendayo kasi yatasimama kulia na kushoto mwa kituo kutegemea na liendako.
Usafiri utakuwa ni bora zaidi kwasababu abiria watalipa nauli kabla ya kupanda basi, watapumzika kwenye kituo bila ya kuunguzwa na jua na barabara ya mabasi hayo yatakuwa yakipita yenyewe tu bila kuingiliana na magari mengine na kutoa fursa ya mwendo wa kasi.
Kuhusu magari mengine kama inavyoonekana pichani pembeni kabisa kutakuwa na barabara kwajili ya magari mengine ya kawaida huku kukiwa na sehemu maalum kwaajili ya kuvuka watembea kwa miguu.
September 8, 2012
PATA UNDANI WA MRADI WA MABASI YAENDAYO KWA KASI UNAOENDELEA KUJENGWA JIJINI DAR ES SALAAM
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!