StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 8, 2012

PICHA NA HABARI YA YANGA WAKITEMBELEA TBL JANA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Mfanyakazi katika Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emmanuel Sawe (kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya viongozi na wachezaji wa timu ya Yanga.


Mfanyakazi wa TBL, Emmanuel Sawe (kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya viongozi wa Yanga.


Wachezaji kwa raha zao.


Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe (kulia) akiwa na kocha wa timu ya Yanga, Tom Saintfiet.


Picha ya pamoja na wafanyakazi wote.

MABINGWA wa Kombe la Kagame Yanga, jana wamefanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Kampuni ya Bia nchini (TBL), kilichopo Ilala jijini Dae es Salaam, ambacho kinaidhanmini klabu hiyo kupitia bia ya Kilmanjaro.

Akiongea katika ziara hiyo, Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu, alisema timu yake iliamua kufanya ziara yao katika kiwanda hicho, ili kuweza kujionea mambo mbalimbali ambayo yanafanywa na kampuni hiyo inayozalisha vinwaji mbali mbali, ikiwamo Kilimanjaro.

Alisema kuwa, Kilimanjaro Premium Lager imekuwa ikiwapa ushirikiano mkubwa katika utekelezaji wa mambo mbalimbali ya kimichezo, ikiwa ni pamoja na kuwapatia magari ya usafiri jezi pamoja na vifaa, na kwamba wamefurahishwa na aina ya mapokezi waliyoyapata kiwandani hapo na kuwaomba waendelee na moyo huo huo wa kuthamini timu yao.

"Tunawaomba muendele na moyo huo huo kwani sisi kama Yanga, tunaamini kuwa huwezi kutenganisha mafanikio ya klabu yetu kwa sasa na udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager, na kwamba kwa pamoja, tutaweza kulifikisha soka la Tanzania katika kilele cha ubora," alisema Sendeu.

Awali, Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema kuwa wamefurahishwa sana na kitendo cha Yanga kuamua kuacha shughuli zao na kutembelea kiwanda chao, kujionea kazi za uzalishaji zinavyofanywa kiwandani hapo.

Alisema kuwa Kilimanjaro Premium Lager inathamini mchango wa timu ya Yanga katika maendeleo ya soka la Tanzania na ndio maana imekuwa ikiidhamini timu hiyo, huku akibainisha kuwa wataendela kuidhamini kwa muda mrefu kadri iwezekanavyo.

Thamani ya udhamini wa Kilimanjaro kwa Yanga unafikia jumla ya dola za Kimarekani 1.5milioni (Shillingi Bilioni mbili za Kitanzania) kwa mwaka. Pesa hizi hutolewa kwa ajili ya shughuli mbali mbali kama kusajili wachezaji wapya wa kimataifa, mabasi, vifaa vya michezo na kukiwezesha Mkutano Mkuu wa Mwaka.

"Tunafanya hivi tukiwa na nia ya kupeleka soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio… Ni dhahiri kuwa Yanga imekuwa ikifanyia mambo makubwa kwani imekuwa ikiwapatia vijana mbalimbali ajira kupitia timu yao.

"Ushirikiano wetu na Yanga unatokana na ukweli kwamba, ni kati ya timu zenye wapenzi wengi zaidi hapa nchini," alisema Kavishe

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat