Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Mwenyekiti wa Chombo Kinachoshughulika na masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika) cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Rais Jakaya Kikwete
Mwenyekiti wa Chombo Kinachoshughulika na masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika) cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Rais Jakaya Kikwete amesema kwamba jumuiya hiyo itakuwa tayari kupeleka jeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) ikiwa hatua hiyo itaelekezwa na Jumuiya ya kimataifa inayoshughulika na migogoro katika ukanda wa Maziwa Makuu.
Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada kumalizika kwa mkutano uliohudhuriwa na marais wanne kwa lengo la kupokea taarifa ya mkutano uliofanywa kati ya mwenyekiti wa SADC na Rais wa Rwanda, Paulo Kagame, kuhusiana na hali ya machafuko inayoendelea katika eneo la mashariki mwa DRC.
Mkutano huo ulioitishwa kwa maelekezo ya mwenyekiti wa SADC, Armando Guebuza, ulihudhuriwa na Guebuza mwenyewe, ikiwa ni pamoja na marais Hifikepunye Pohamba wa Namibia, Joseph Kabila wa DRC; Kikwete wa Tanzania; Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini, Novisiwe Maphisa-Nqakula aliyemwakilisha rais Jacob Zuma na Katibu mkuu mtendaji wa SADC, Dk. Tomaz Salomao.
Rais Kikwete alisema mkutano huo wa Troika umeikaribisha ripoti ya mwenyekiti huo na kuafiki mapendekezo yote aliyoyatoa kufuatia mazungumzo aliyoyafanya na Kagame kuhusiano na vita inayoendeshwa na kikundi cha M23 kwa kuwa yanalenga kuimaliza vita hiyo.
September 5, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!