StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 21, 2012

SAINTFEIT ANASEMA NINI BAADA YA KIPIGO CHA 3-0?

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Akizungumza baada ya mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika Uwanja wa Kaunda Dar es Salaam asubuhi jana, Saintfiet alisema Yanga ingeweza kuibuka na ushindi kama washambuliaji wake wangetumia vizuri nafasi nane walizopata kwenye mechi hiyo.
“Sisemi kama wangetumia nafasi zote walizopata, lakini wangetumia baadhi ya hizo tungeweza kushinda mechi hiyo, pia tulipata penalti ambayo tulikosa,”alisema Saintfiet.
Washambuliaji wa Yanga juzi walikuwa ni Hamisi Kiiza na Said Bahanunzi, ambapo Kiiza pia alipoteza penalti.
Alikanusha kupenda kutumia mfumo wa kujihami ambao wachambuzi wa soka wanasema ndio chanzo cha kuinyima timu hiyo ushindi kwenye mechi zake, kwa kusema alicheza na washambuliaji wawili kwenye mchezo huo na ndio maana waliweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga.
Saintfiet alisema pia safu yake ya ulinzi ilijichanganya kwenye mechi hiyo kiasi cha kuruhusu mabao mawili ya kwanza na kusema bao la tatu la Mtibwa lilifungwa kwa mkwaju wa mbali na hivyo anaona kama lilitokana na ubovu wa mabeki wake kutojipanga sawasawa.
“Tuna mabeki bora Afrika lakini mabao mawili ya kwanza yalitokana na kujichanganya kwao, bao la tatu lilifungwa kwa shuti la mbali,”alisema Saintfiet.
Pia aliendelea kuilalamikia ratiba ya Ligi Kuu kwani inaipendelea sana Simba kwa kucheza mechi tatu zote nyumbani na wao kucheza mechi mbili ugenini, ingawa alisema wanajipanga kwa ajili ya mchezo dhidi ya JKT Ruvu ambao amesema utakuwa mgumu lakini wamejiandaa kushinda kujiweka kwenye msimamo mzuri kwenye ligi.
Kocha huyo alisifu mazingira ya hoteli waliyofikia mjini Morogoro kuwa ilikuwa na huduma nzuri za maji, chakula na kila mchezaji alilala kwenye chumba chake tofauti na hoteli waliyofikia Mbeya ambapo alidai wachezaji walilazimika kulala wawili kwenye kitanda kimoja.
Timu hiyo ilirejea Dar es Salaam jana asubuhi ikitokea Morogoro na moja kwa moja wachezaji walienda mazoezini.
Wakati huohuo, Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic amelalamikia kadi nyekundu aliyeoneshwa mshambuliaji wa timu hiyo, Emmanuel Okwi kwenye mechi dhidi ya JKT Ruvu juzi, ambayo Simba ilishinda mabao 2-0.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Milovan alisema mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda alis tahili kuoneshwa kadi ya njano kutokana na kosa hilo na siyo kadi nyekundu.
“Nimefurahi kupata pointi tatu muhimu, mchezo ulikuwa mgumu lakini wachezaji wangu walicheza vizuri na kupata matokeo,”alisema Milovan.
Okwi mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo alioneshwa kadi nyekundu kwa kumpiga kiwiko beki wa JKT Ruvu, Kessy Mapande akiwa hana mpira baada ya muamuzi Andrew Shamba kuamuru faulo ipigwe kuelekea lango la JKT Ruvu na ndipo Okwi alimfuata mchezaji huyo na kumpiga kiwiko hali inayomuweka kwenye wakati mgumu wa kufungiwa mechi tatu kutokana na kanuni za ligi hiyo.
Kwa upande wake kocha wa JKT Ruvu Charles Kilinda alisema kadi aliyooneshwa mshambuliaji huyo ilikuwa halali kwani ni dhahiri alimpiga kiwiko beki wa timu yake.
Kuhusu mchezo Kilinda alisema timu yake iliruhusu mabao ya kizembe na kusema sasa wanajipanga na mchezo dhidi ya Yanga Jumamosi.


Tom Saintfiet
KIPIGO cha mabao 3-0 ilichokipata Yanga juzi kutoka kwa Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri Morogoro bado kinamtesa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Tom Saintfiet huku akiwalaumu washambuliaji wake kwa kutokuwa makini.
MSIMAMO LIGI KUU BARA
Na   Timu                      P  W  D  L  GD  Pnt
1    Simba SC                2   2   0  0   5    6
2    Mtibwa Sugar          2   1   1   0   3   4
3    Azam FC                 2   1   1   0   1   4
4    Coastal Union          2   1   1   0   1   4
5    Shooting                 2   1   0   1   0   3
6    JKT Ruvu                 2   1   0   1  -1   3
7    African Lyon            2   1   0   1  -2    3
8    Toto Africa              2   0   2   0   0    2
9    Prisons FC               2   0   2   0   0    2
10  JKT Oljoro               2    0   2   0   0    2
11  Kagera Sugar          2    0   1   1  -1    1
12  Polisi                      2    0   1   1  -1    1
13  Yanga                     2   0    1   1  -3    1
14  Mgambo                 2   0    0   2   -2   0

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat