Rais wa MarekaNi Barack Obama amelaani vikali shambulizi lililofanywa dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Benghazi Libya hapo jana.
Katika taarifa ya Obama iliyothibitisha kuuawa kwa balozi huyo, Christopher Stevens, pia ilisema wamerekani wengine watatu waliuawa wakati wa shambulio hilo.
Ubalozi uliteketezwa na watu waliokuwa wamejihami kwa makombora na maguruneti wakati wa maandamano ya kulaani filamu ya Marekani ambayo walisema ilimkejeli Mtume Muhammed.Spika wa bunge Mohammed Magarief, ameomba radhi kwa Marekani kufuatia mashambulizi hayo na mauaji yaliyofuata.
Chanzo: http://www.bbc.co.uk/swahili/news
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!