StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

September 10, 2012

TRENI YAWAKA MOTO MANYONI, ABIRIA 15 WAJERUHIWA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Abiria wapatao 15 walijeruhiwa kutokana na taharuki iliyotokea baada ya kichwa cha treni kimoja kati ya viwili vilivyokuwa vinapandisha treni ya abiria kushika moto kati ya maeneo ya Stesheni za Saranda na Manyoni juzi Septemba 8, 2012 majira ya saa moja jioni. Taharuki hiyo ilisababisha abiria kuanza kuruka nje pamoja na kukanyagana.

Majeruhi wanane waliruka kutoka behewa lililokuwa karibu na vichwa vya treni wakati wengine saba walitoka katika mabehewa mengine 14.

Hali hiyo iliweza kudhibitiwa pale Dereva na wasaidizi wake walipofanikiwa kusimamisha treni na kutenganisha vichwa hivyo na mabehewa ya abiria ambapo kichwa kilichokuwa kimeshika moto kilikokotwa hadi stesheni ya Manyoni mnamo saa 01:15 usiku. Baada kufanikiwa kukizima kichwa kilichokuwa kinawaka saa 1:45 usiku kichwa kizima cha treni kilirejea eneo la tukio na kuyavuta mabehewa ya abiria na kuwasili Stesheni ya Manyoni saa 3:15 usiku ambako uhakiki wa abiria waliojeruhiwa ulifanyika.

Abiria 15 waliojeruhiwa walikimbizwa hospitali ya Manyoni ambako baada ya uchunguzi abiria wawili walikutwa na majeraha makubwa. Majeruhi hao wametambuliwa kwa majina kuwa Bwana Bartholomew Raphael aliyevunjika mkono wa kushoto na Bibi Sikujua Mtonzi aliyevunjika mguu wa kulia. Majeruhi hawa wamehamishiwa hospitali kuu ya Mkoa wa Dodoma. Wengine 13 walitibiwa na kuruhusiwa kuendelea na safari .

Treni iliondoka Manyoni saa 7: na dakika 40 usiku na iliwasili Stesheni ya Tabora saa 3 na dakika 30 jana asubuhi hii na imeondoka saa 5 na dakika 30 asubuhi kuelekea Kigoma ambapo iliwasili salama saa 5: 05 usiku hapo jana.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat