Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
MPIRA tena basi mimi! Ndivyo alivyosikika mshambuliaji wa Coastal Union, Nsa Job akilia kwa uchungu alipokuwa akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuteguka mguu wa kushoto baada ya kugongana na kipa wa JKT Ruvu, Patrick Muntari katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Chamazi.
Aliumia sehemu ya chini ya goti na kusababisha mguu kupinda lakini amefanyiwa matibabu na kuwekewa bandeji ngumu (P.O.P).
Ilikuwa katika dakika ya 66, Nsa alipokuwa akifanya mashambulizi kwenye lango la Kaskazini la uwanja na kukutana uso kwa uso na Muntari.
Tukio hilo liliibua madudu ya udhaifu wa uendeshaji wa Ligi Kuu kwa mechi ambazo hazifanyiki Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Hakukuwa na gari la wagonjwa (ambulance) hali iliyosababisha mchezaji huyo asote uwanjani hapo kwa zaidi ya nusu saa huku ukitafutwa usafiri wa kumfikisha hospitali baada ya kupatiwa huduma ya kwanza.
Hata hivyo, huduma ya kwanza aliipata katika zahanati ya klabu ya Azam ambayo timu hiyo huitumia kuwahudumia wachezaji wake wanapopata matatizo.
Inashangaza kuona mechi za ligi zinachezwa bila kuwepo kwa gari la wagonjwa na kuna siku maafa makubwa zaidi yanaweza kutokea katika viwanja vya soka.
Hata hivyo, baada ya Nsa kupata huduma ya kwanza, alipelekwa Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI) kwa msaada wa gari binafsi huku wakisindikizwa na gari la polisi ili kukwepa msongamano wa magari.
Nsa anavyoelezea
"Ilikuwa mbaya, nimelia sana nilikuwa nasikia maumivu makali mno kwenye mguu na niliteseka zaidi barabarani nilipokuwa nakwenda hospitalini pale gari ilipokuwa likidunda kwenye mashimo,"anasema Nsa ambaye alishuhudiwa na Mwanaspoti katika chumba cha huduma ya kwanza akilia maumivu kama mtoto.
"Lakini kilio kingine nilikuwa nawaza maisha yangu, huenda mpira kwangu ndiyo basi tena kila nilipokuwa nauangalia mguu wangu ulivyopinda, lakini nashukuru kwa sasa baada ya kupatiwa matibabu maumivu yamepungua,"anaeleza Nsa, ambaye alikaa MOI kwa saa nne juzi Jumapili usiku akipatiwa matibabu na baada ya hapo alirudishwa kwenye hoteli iliyofikia ili kujiunga na wenzake.
October 30, 2012
Ajali ya kutisha ya Nsa Job!
Millionfortune.com
MICHEZO
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!