Waya wa Baharini utakaotumika katika Mradi wa ulazaji waya wa pili wa Umeme kutoka Ras-Kiromoni Dar es Salaam hadi Ras-Fumba Zanzibar,wenye urefu wa 37 Kilomita, katika Bandari ya Malindi ukiwa katika Meli ya Kampuni ya Viscas kutoka nchini Japan
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, alipokuwa akisalimiana na Msaidizi Mtendaji Mkuu wa MCA-T kwa upande wa Zanzibar, Bw,Ahmed Rashid,alipowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja leo,kuupokea na kuukagua waya huo wa Umeme ,utakaolazwa kwa siku Kumi na mbili kutoka Ras-Kiromoni Dar es Salaam hadi Ras-Fumba Zanzibar. [Picha na Ramadha
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,( kushoto) akifuatana na Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati,Ramadhan Abdalla Shaaban,alipofika katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja leo,Kuupokea na Kuukagua Waya wa Baharini utakaotumika katika Mradi wa Ulazaji waya wa pili wa Umeme kutoka Ras-Kiromoni Dar es Salaam hadi Ras-Fumba Zanzibar,ukiwa katika Meli ya Kampuni ya Viscas kutoka nchini Japan.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Zanzibar Hassan Ali Mbarouk akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya Rais Dk Ali Mohd Shein kuupokea Waya Mpya wa Umeme wenye uwezo wa kuchukua Megawati 100.kutoka Tanzania Bara hadi Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!