Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba
Wakati ulimwengu ukiadhimisha ‘Siku ya Walimu Duniani’ leo, walimu wa Tanzania hawatakuwa na maadhimisho yoyote kutokana na madai yao kutotimizwa pamoja na ahadi, ambazo wamekuwa wakiahidiwa na serikali kila mwaka kwa miaka sita sasa.
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, alisema tofauti na miaka mingine wataadhimisha siku yao wakiwa kazini na wakiwa wamekata tamaa kutokana na mwajiri wao, ambaye ni serikali kushindwa kuwatimizia madai yao ya msingi.
Alisema madai yao kwa serikali, ambayo hayajatimizwa hadi sasa, ni kuboreshewa mazingira ya kazi, nyongeza ya mishahara inayokidhi hali halisi kwenye utumishi wa umma pamoja na kuongezwa posho ya kufundishia.
Aliitaka serikali kukubali ushauri wa Bunge na uamuzi wa Mahakama ya Kazi uliozitaka pande mbili kukaa kwenye meza ya majadiliano ili kuendeleza mazungumzo ya namna ya kutatua mgogoro uliopo unaohusu madai ya walimu nchini.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!