StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

November 5, 2012

HIVI NDIVYO JUSTIN TIMBERLAKE NA JESSICA BIEL WALIVYOKULA FUNGATE LAO NCHINI TANZANIA

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
Wanandoa wapya walioana mbele ya ndugu na jamaa zaidi 100 kwenye hoteli ya Borgo Egnazia ya mjini Puglia, kusini mwa Italia October 19 hivi karibuni walichukua ndege binafsi na kuingia nchini kupitia uwanja wa ndege wa KIA kabla ya kuelekea katika reserve yenye hoteli za kifahari ya Singita Grumeti iliyopo katika mbuga ya wanyama ya Serengeti.

Kwa mujibu wa mtandao wa MailOnline, staa huyo na mke wake walitumia siku zake za mwanzoni nchini akiwa Sasakwa Lodge.

Wanadaiwa pia kukaa Faru-Faru Lodges katika hifadhi hizo zenye ukubwa heka 350,000 kwa siku kadhaa kabla ya kuondoka October 30 kwa helicopter.


Wapenzi hao pia wanadaiwa kuchukua ndege binafsi kuzunguka katika beach ya hoteli hiyo kabla Jessica hajaanza kushoot video yake mpya ‘The Devil and the Deep Blue Sea’.

Justin anatararajia kufanya ziara nyingine nchini Tanzania siku za mbeleni ambapo ataungana na Lupe Fiasco kupanda mlima Kilimanjaro.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat