StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

November 12, 2012

POLISI: USALAMA BARABARANI YAKUSANYA BILLION 11 NDANI YA MIEZI 8

Tweeted this Like this, be the first of your Friends Jeshi la Polisi kitengo la Usalama Barabarani nchini, kimekusanya zaidi ya Shilingi bilioni 11 katika kipindi cha Januari hadi Septemba mwaka huu kutokana na makosa 388,700 yaliyofanywa na madereva wa magari.

Akizungumza na NIPASHE juzi, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, SACP Mohamed Mpinga, alisema kiasi hicho kimetokana na kutozwa faini kwa madereva waliopatikana na hatia ya uendeshaji wa uzembe, ubovu wa magari pamoja na makosa mengine.

“Tumekusanya sh.11,975,008,000 kwa kipindi cha miezi tisa tu mwaka huu, hiyo inaonyesha ni jinsi gani madereva wengi wasivyozingatia usalama wa barabara na kuhatarisha usalama wa watumiaji wengine,” alisema SACP Mpinga.

Kamanda Mpinga alisema kiasi hicho ni tofauti ukilinganisha na faini iliyopatikana mwaka uliopita ya zaidi ya sh. bilioni tisa kutokana na makosa 369,800 yaliyofanywa na madereva kwa kutozingatia sheria za barabarani.

Alisema makusanyo ya faini ya mwaka jana yalikuwa sh.9,029,540,000.

Hata hivyo, Kamanda Mpinga alisema makusanyo hayo ni pesa zinazoingia katika mfuko wa serikali, huku akiwasisitizia madereva na wamiliki wa magari kuzingatia ubora wa magari yao pamoja na kuendesha kwa kufuata sheria za usalama barabarani.

Katika hatua nyingine, Kamanda Mpinga aliwashauri madereva wanaokamatwa na kutozwa faini kutokana na makosa mbalimbali barabarani, iwapo wataamini hawajatendewa haki waende kutoa taarifa kwa Afisa wa Usalama Barabarani wa Mkoa (RTO) ili walalamike huko kuliko kunung’unika… kwani vitabu vya malipo ya adhabu ni vile viliyotangazwa na gazeti la serikali no.257 ya Agosti 2011 na si vinginevyo, alisema.

Pia Kamanda Mpinga alisema vitabu vya adhabu, haviruhusiwi kushikwa na askari ambaye hana cheo zaidi ya mwenye cheo cha koplo na sajenti, hivyo kuwaandikia makosa madereva wakati askari hana cheo ni kosa.

SACP Mpinga alisema kikosi cha usalama barabarani kimeanzisha utaratibu wa kupokea faini papo kwa hapo kutokana na madereva wengi kutokuwa waaminifu pale wanapokutwa na makosa na kisha kuachiwa ili wapelekee baadaye kulipa.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat