Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Mchakato wa kuendelea kuitambulisha huduma ya Airtel Supa5 mikoani
utaendelea mwishoni mwa wiki hii ambapo Airtel itaweka kambi mkoani
Mwanza katika viwanja vya wazi vya Furahisha vilivyopo jijini Mwanza.
Akizungumzia tamasha hilo la kuitambulisha SUPA5 mkoani Mwanza Afisa
Uhusiano wa Airtel, Bi Jane Matinde alisema lengo la kuunganisha
utambulisho huu burudani ni kuwavutia vijana na wateja wengi kuhudhuria
na kujifunza faida lukuki za SUPA5 ili waitumie zaidi.
Tamasha linafanyika kwa siku mbili mfululizo ambapo siku ya Jumamosi
tunatoa fulsa kwa wasanii chipukizi kujitokeza kwa wingi kuonyesha
vipaji vyao sambamba na kupata huduma ya Airtel SUPA5.
Jumapili itakuwa uzinduzi kamili ambapo wasanii wakubwa watatoa
burudani BURE, akiwemo Juma Nature na kundi zima la Wanaume Halisi,
Mwasiti a.k.a SOJA, Roma Mkatoliki a.k.a mzee wa tuzo kibao watatoa
burudani kali kwa wateja watakaohuduria tamasha hilo BURE.
Bi Matinde pia amezungumzia lengo la huduma ya dili tano bomba
zilizopo kwenye huduma ya SUPA5 kuwa Airtel inatimiza dhamira yake
iliyojiwekea ya kufikisha na kupunguza gharama za mawasiliano nchini
kote bila kuwasahau vijana na wanafunzi kunufaika kwa kupata internet
bure wakati wa usiku, kutuma sms bure na faida nyingine nyingi.
Huduma ya Airtel SUPA5 ilizinduliwa rasmi siku za karibuni jijini Dar
es Salaam kisha kufuatiliwa na kufanyika kwa matamasha ya burudani ya
BURE katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Iringa, Arusha huku mwishoni mwa
wiki hii itakuwa zamu ya wakazi wote wa Mwanza.
Wasanii mahiri waliokwishapamba majukwaa ya Airtel SUPA5 hadi sasa
kwa mkoa wa Dar es salaam ni Fid Q, Mwasiti, Godzilla, pamoja na Kundi
la Tip Top Connection akiwemo Madee, Tundaman, Richard na Dogo Janja kwa
mkoa wa IRINGA ni Juma Nature na kundi zima la Wanaume Halisi, Roma
Mkatoliki, pamoja na Kundi la Tip Top Connection akiwemo Madee, Tundaman
na Richard. Mkoa wa Morogoro na Dodoma ni kundi mahiri la Wanaume
Family likiongozwa na Chegge na Temba na kukamilisha ladha ya zaidi kwa
kuwepo kwa Bendi Maarufu jijini ya Mashujaa ikiongozwa na kingunge
Charles Baba na wasanii wengine.
June 19, 2012
JUMA NATURE, ROMA NA MWASITI KUFUNIKA TAMASHA LA AIRTEL SUPA5 MWISHONI MWA WIKI HII MWANZA
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!