Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
KUNA habari kwamba mama wa
marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa, ‘picha haziendi’ na mwigizaji wa
filamu za Kibongo, Irene Uwoya kutokana na mama huyo kudai fedha za
rambirambi kwa Uwoya alizodai amezila.
Hivi karibuni Uwoya na wenzake
Patchou Mwamba na Juma Chikoka ‘Chopa’ walikuwa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo kumalizia msiba wa swahiba wao huyo.
Akizungumza na Risasi
Mchanganyiko hivi karibuni, Chopa aliyekuwa miongoni mwa walikuwa nchini
humo, alisema kuwa baada ya kurejea nchini, mama Kanumba aliwataka
waende nyumbani kwake na fedha za rambirambi walizopewa kama pole wakiwa
Kongo, jambo lililoshangaza sana.
“Sisi tulikwenda Kongo kwa heshima
ya marehemu Kanumba na pia kuendeleza uhusiano mzuri aliokuwa ameanza
kuutengeneza ndiyo maana wengine wamejilipia nauli. Kutudai rambirambi
kumetushangaza sana, anategemea hizo fedha zitatoka wapi?” alisema Chopa
kwa mtindo wa kuhoji.
Kwa upande wa Uwoya, alipoulizwa kuhusu ishu
hiyo, alikiri kuwa ni kweli amesikia kuwa mama Kanumba anadai rambirambi
za msiba wa mwanaye kwa wasanii waliokuwa nchini Kongo akiwemo yeye na
kueleza masikitiko yake.
“Sasa mama Kanumba anategemea hizo fedha
tunazitoa wapi? Hajui jinsi tulivyopata shida ya usafiri wa kwenda na
kurudi, wengine tumelazimika kujigharamia wenyewe nauli, hii yote ikiwa
ni kumuenzi mwenzetu, sasa yeye anadai fedha za kutoka wapi?” alihoji
Uwoya.
Baada ya kusikia kutoka upande mmoja wa wasanii waliokwenda
Kongo, Risasi Mchanganyiko lilitenda haki kwa kutafuta mzani wa madai
hayo kutoka upande wa pili, likamvutia waya Mama Kanumba ambaye alitoa
ushirikiano.
Mama Kanumba alisema, ameshangazwa sana kusikia kuwa
Uwoya na wenzake wamesafiri kwenda Kongo kwa ajili ya kumalizia msiba wa
mwanaye bila kumpa taarifa akahoji; Nani amewapa ruksa ya kufanya
hivyo?
“Nimesikia wamekwenda Kongo kumalizia msiba wa mwanangu lakini
mpaka sasa sijajua mwanafamilia gani aliyewapa ruksa ya wao kwenda
huko. Pia sijapewa chochote walichorudi nacho kutoka huko.
“Uwoya na wenzake walete pesa za rambirambi za mwanangu walizopewa Kongo vinginevyo hatutaelewana,” alisema Mama Kanumba.
UHUSIANO WA UWOYA, PATCHOU, CHOPA NA KANUMBA
Kwa namna moja au nyingine, Uwoya na Patchou Mwamba walisaidiwa sana kuingia katika sanaa ya uigizaji na marehemu Kanumba.
Uwoya alitokea kwenye tasnia ya urembo na Patchou akiwa ni mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia, kazi anayoifanya hadi sasa.
Kwa
upande wa Chopa, alianza kujuana na Kanumba tangu wakiwa pamoja katika
Kundi la Kaole Sanaa. Ukaribu wao na marehemu ndiyo uliowafanya wasafiri
hadi nchini Kongo kumalizia msiba wa swahiba wao huyo.Chanzo:www.globalpublishers.info
June 20, 2012
MAGAZETINI LEO:UWOYA KALA RAMBIRAMBI ZA KANUMBA
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget