Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
MWILI wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Willy Edward
Ogunde, unatarajiwa kuagwa leo kuanzia Saa 4:00 asubuhi kwenye Viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Willy alifariki ghafla usiku
wa kuamkia Jumapili mjini Morogoro, baada ya kuanguka kwa kile
kilichodaiwa kuwa ni kutokana na maradhi ya moyo.
Kwa mujibu wa
taarifa ya familia ya mzee Edward Ogunde, baada ya mwili huo kuagwa,
utasafirishwa kwenda Mugumu, Serengeti, Mara kwa ajili ya mazishi
yanayotarajiwa kufanyika Juni 23, mwaka huu.
“Msiba upo nyumbani kwa
kaka yake mkubwa, ndugu Denis Ongiri eneo la Mburahati-Msikitini jijini
Dar es Salaam. Mazishi yatafanyika nyumbani kwao kitongoji cha
Morotonga, Mugumu, Serengeti,” ilisema Taarifa hiyo.
June 20, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!