Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania( TanTrade), imetangaza
viingilio vipya vya watu na magari katika maonyesho ya kimataifa ya
Sabasaba ambapo watu wazima watalipa Sh 2,500 na watoto Sh 500.
Viingilio
hivyo vimeelezwa kuwa vitatumika siku zote isipokuwa siku maalumu ya
Juni 7, ambapo viingilio vitakuwa Sh 3,000 kwa watu wazima na watoto Sh
1,000.
Pia, imetangaza viingilio vya magari kuwa tiketi za kupaki magari madogo kila siku ni Sh4,000 na malori ni Sh40,000.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na mdhamini rasmi wa mawasiliano wa
maonyesho hayo kampuni ya Vodacom Tanzania,Tan Trade imetangaza kuwa
maonyesho hayo yataanza rasmi Juni 28 hadi Julai 8, mwaka huu.
Kwa
watakaohudhuria maonyesho hayo na magari madogo watatakiwa kununua
tiketi kwa Sh 4,000 kama ambavyo mchanganuo wa malipo unavyobainisha
malipo ya huduma nyingine zikiwamo za kupaki magari kama malori na
magari makubwa pamoja na huduma nyingine.
Maonyesho ya kimataifa
ya Dar es salaam ni maonyesho pekee yanayoongoza katika huduma za masoko
Tanzania, maonyesho hayo yanayodumu kwa siku kumi, huvutia watazamaji
zaidi ya laki tatu na nusu na kutoa fursa kwa kampuni kuonyesha bidhaa
zao na wanaohudhuria kupata nafasi ya kuuliza maswali na kulinganisha
ubora wa bidhaaa zilizopo.