Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
WAREMBO wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss Dar Intercollege
2012 Jumatano ya kesho wanatarajiwa kujivinjari katika ukumbi wa
kimataifa wa Club Bilicanas iliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Shindano hilo limepangwa kufanyika Ijumaa ya Juni 22 katika ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa uliopo mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)
ambapo msanii wa bongo Fleva Naseeb Abdul ‘Diamond’ anatarajiwa
kutumbuiza.
Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail amesema leo kwamba, warembo hao
watapata kuhudhuria onyesho maalum la bendi ya African Stars "Twanga
Pepeta' kupitia usiku wa Mwafrika unaorindima kila Jumatano katika klabu
hiyo.
Dina alisema uongozi wa Bilicanas Group umewaalika warembo hao ili
kuweza kuburudika pamoja na mashabiki wa muziki wa dansi nchini kwa
lengo la kujipoza baada ya mazoezi yao.
"Warembo wetu wamealikwa kesho pale Bilicanas ambapo bendi ya Twanga
Pepeta hutumbuiza kila Jumatano kupitia usiku wa Mwafrika, hivyo
tunaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwashuhudia kabla ya kuja tena
Ijumaa katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa,"Alisema.
Alisema maandalizi ya shindano hilo yanakwenda vema ambapo warembo 14
watakaoshiriki wanaendelea na mazoezi katika hoteli ya The Grand Villa
iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
“Mwaka huu tumejipanga vema
kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema
katika fainali za Miss Tanzania,” alisema Dina.
Warembo
watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi
wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha (IFM) na
Chuo Kikuu huria (OUT) ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka
IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali
za Miss Tanzania.
Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na
Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana
Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa
Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano
hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya
Redd’s, Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band, Lamada Hotel,
Screen Masters, Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions,
Lamada Hotel, Grand Villa Hotel, Sporti Kizaa zaa, Clouds Fm na blog za
Michuzi, Dinaismail (zamani Mamapipiro), Bin Zubeiry, Mtaa kwa Mtaa na
Fullshangwe.
June 19, 2012
WAREMBO MISS DAR INTERCOLLEGE KUSUGUA KISIGINO CHA TWANGA, CLUB BILICANAS KESHO
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!