Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
KLABU ya Tottenham Spurs ipo mbioni kumnunua moja kwa moja
mshambuliaji Emmanuel Adebayor kutoka Manchester City kwa dau la Pauni
5 milioni kwa mujibu mtandao wa Goal.com.
Klabu hiyo ya London
imepunguza dau wanalotaka City mara mbili na kudai ipo tayari kutoa
Pauni 5 mil kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa Togo, pia wanaangalia
uwezekano wa kupunguza mshahara wake wa sasa wa Pauni 170,000 kwa wiki.
Chanzo
cha habari kutoka City kilisema wanategemea uhamisho huo utakamilia na
kujiweka vizuri kwa ajili ya mpango wao wa kutaka kumsajili nahodha wa
Arsenal, Robin van Persie.
Mabingwa hao wa England walitegemea
kumuuza Adebayor kwa dau kubwa msimu huu kutokana na awali Paris
Saint-Germain na AC Milan kuonyesha nia ya kumtaka, lakini sasa
Tottenham imekuwa ni timu pekee yenye nia naye.
Adebayor, 28,
ameweka wazi nia yake ya kutaka kucheza White Hart Lane chini ya kocha
mpya Spurs, Andre Villas-Boas ambaye pia ameonekana kuvutiwa na
mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal.
“Tunataka jambo hili
limalizike kwa haraka huku pande zote City, Spurs na mchezaji mwenyewe
akilizika na hilo,” chanzo hicho kiliimbia Goal.com. “Spurs ndiyo timu
pekee iliyokuja kwa ajili ya kufanya mazungumzo juu yake na City ipo
tayari kumwachia.”
Adebayor alikuwa na mchango mkubwa kwa
Tottenham msimu uliopita alipokuwa akicheza kwa mkopo chini ya kocha
Harry Redknapp, akiwa amefunga mabao 17 katika Ligi Kuu na kutegeneza
mengine 11 katika mechi 33 alizocheza, pia amekuwa na ushirikiano mzuri
na winga Gareth Bale.
Uwepo wake utakuwa ni faida kubwa kwa kocha Villas-Boas anayetegemea kuanza kibarua chake leo kujindaa na msimu mpya.
Adebayor
alisajiliwa na City kwa mkataba wa miaka mitano akitokea Arsenal mwaka
2009 kwa gharama ya pauni 25m, lakini hakuwa na wakati mzuri ndani ya
uwanja wa Etihad tangu alipoteuliwa Roberto Mancini kuifundisha timu
hiyo Desemba 2009.
Wakati huohuo; Fiorentina ipo tayari kutoa pauni 4milioni kwa ajili ya mshambuliaji wa Arsenal, Marouane Chamakh.
Mshambuliaji huyo wa Morocco amefunga mabao 12 katika mechi 63 alizocheza Gunners.
Vyanzo vya karibu na mchezaji huyo vimedai: “Kuwa klabu hiyo ya Italia imeonyesha nia kubwa ya kutaka kumsajili.”
July 9, 2012
Adebayor auzwa kwa bei poa Spurs
Millionfortune.com
BURUDANI
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!