Wachezaji wa timu ya Tanzania inayokwenda kushiriki michezo ya Olimpiki wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuondoka majira ya saa kumi jioni kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda London, Uingereza.
Muogeleaji
wa mita 100 wa Tanzania Magdalena Moshi akiwa na kaka yake (kushoto)
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere muda mfupi kabla
ya kuelekea London, Uingereza katika michezo ya Olimpiki.
Kocha wa Riadhaa, Zakaria Ngwandu muda mfupoi kabla ya kuondoka
Mkurugenzi
wa Michezo Tanzania, Leonard Thadeo, akiwaasa wachezaji kujituma katika
michezo hiyo huku akisisitza kuwa na nidhamu kwa muda wote wa kambi
na mashindano
DAR ES SALAAM, Tanzania
TIMU
ya Tanzania inayokwenda kushiriki michezo ya Olimpiki imeondoka
leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda London,
Uingereza, huku ikiwa na matumaini ya kurudi na medali.
Timu hiyo ya Tanzania yenye wanamichezo sita ambao ni wa Kuogelea, Ngumi za Riadhaa na Riadha imeondoka jana majira ya jioni kushiriki michuano hiyo inayoanza Julai 27 hadi Agosti 12 mwaka huu, yakishirikisha nchi 205.
Akizungumza
muda mfupi kabla ya kupanda ndege, mmoja wa wachezaji hao, bondia wa
ngumi za ridhaa, Seleman Kidunda, amejinasibu kufanya maandalizi ya
kutosha kumuwezesha kurudi na medali, ingawa pia aliomba dua za
Watanzania.
“Naenda
kulipigania taifa kuhamasisha mabondia ambao wanadhani kuwa Tanzania
haiwezi. Lengo ni kuitangaza nchi na Afrika, hasa ukizingatia kuwa haya
ni mashindano makubwa duniani. Muhimu kwa Watanzania kutuombea dua,”
alisema Kidunda.
Kwa
upande wake, Kocha wa ngumi, Mrakibu wa Magereza, (SP), Remmy Ngabo,
alisema amempa Kidunda mazoezi ya kutosha na anaamini yatamsaidia kwenye
mashindano hayo yanayoanza kuanza
Mwanariadha wa Marathon, Zakia Mrisho alisema kwa upande wake anaenda London kwa nia moja tu ya kurudi na ushindi na kwamba hakutakuwa na kisingizo cha maandalizi, kwania amefanya ya kutosha kumpa medali.
Aidha
akizungumza wakati wa kuiaga timu hiyo, Mkurugenzi wa Michezo Tanzania,
Leonard Thadeo, amewaasa wachezaji hao kujituma katika michezo hiyo
huku akisisitza kuwa na nidhamu kwa muda wote wa kambi na wa mashindano.
Aliongeza kuwa, mashindano hayo yatakuwa na ushindani mkubwa, hivyo wanapaswa kujituma zaidi ili waweze kurejea na medali.
Wanamichezo waliondoka jana ni Zakia Mrisho, ambaye ni mwanariadha anayekimbia mita 5000, Selemani Kidunda ngumi za Ridhaa, Samson Ramadhan, Riadha, Msenduki
Mohmed na Faustine Mussa ambaye anakimbia marathon.
Aliongeza kuwa, mashindano hayo yatakuwa na ushindani mkubwa, hivyo wanapaswa kujituma zaidi ili waweze kurejea na medali.
Wanamichezo waliondoka jana ni Zakia Mrisho, ambaye ni mwanariadha anayekimbia mita 5000, Selemani Kidunda ngumi za Ridhaa, Samson Ramadhan, Riadha, Msenduki
Mohmed na Faustine Mussa ambaye anakimbia marathon.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!