Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
BURUNDI imemtunukia Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, tuzo
ya juu ambayo huitoa kwa watu mbalimbali kutokana na mchango wao katika
kuleta uhuru na amani kwa taifa hilo.
Taarifa iliyotolewa na
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais-Ikulu jana, imeeleza kuwa Mwalimu
Nyerere alitunukiwa Tuzo ya Taifa la Burundi (Order of the National
Republic of Burundi), katika kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 50
ya Uhuru wa Burundi zilizofanyika juzi.
Tuzo hiyo kwa Mwalimu
Nyerere imepokelewa kwa niaba yake na Rais Jakaya Kikwete aliyekuwa
mmoja wa viongozi sita wa nchi za nje waliohudhuria sherehe hizo.
Akitangaza
utoaji tuzo hiyo, Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza alisema kuwa
Burundi imeamua kumtunuku Mwalimu Nyerere kutokana na sababu mbili
akitaja moja ni ushauri wake katika kuleta Uhuru wa Burundi kutoka kwa
wakoloni wa Kibeligiji.
“Kwanza Mwalimu alikuwa mshauri muhimu
sana wa mwanzilishi wa taifa letu, Louis Rwagasore na baadaye zilikuwa
ni jitihada zake ambazo hatimaye zimeleta amani na utulivu, ambao
tunaufurahia katika Burundi kwa sasa,”alisema.
Pamoja na Hayati
Mwalimu, aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela pia ametunukiwa
tuzo hiyo. Mandela alichukua nafasi ya Mwalimu Nyerere kama mpatanishi
wa mgogoro wa Burundi kufuatia kifo cha Nyerere mwaka 1999.
Katika
sherehe hizo, zilizoendelea mfululizo kwa saa saba tokea saa nne
asubuhi hadi saa 11 jioni, Rais Kikwete aliungana na viongozi wenzake wa
nchi sita na wawakilishi wa nchi nyingine nyingi duniani kuhudhuria
kilele cha sherehe hizo za miaka 50 ya Uhuru wa Burundi ilioupata kutoka
kwa wakoloni wa Kibelgiji Julai 2, mwaka 1962.
Mbali na Rais
Kikwete marais wengine waliohudhuria ni Mwai Kibaki wa Kenya, Theodore
Obing Nguema wa Equatorial Guinea, Joseph Kabila wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Francois Bozize wa Jamhuri ya Afrika ya
Kati.
July 4, 2012
Burundi yampa tuzo Mwalimu Nyerere
Millionfortune.com
SIASA
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget