NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), anayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa, Dkt. Julius Rotich (pichani) anataraji kufungua mafunzo ya siku tatu ya upigaji picha yajulikanayo kama ‘EAC-GIZ Master Class Photographers Training’ yatakayo anza Julai 23-26, 2012 mjini Arusha.
Juma
la wapigapicha 10 kutoka nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki
wanataraji kuhudhuria mafunzo hayo ya siku tatu ya Upigaji
yatakayofanyika katika Hotel mjini Arusha.
Mafunzo
hayo ya nadharia na vitendo yameandaliwa kwa ushirikiano kati ya Jumuia
ya Afrika Mashariki na Shirika la Kijerumani (EAC) na GIZ yatahusiha
wapigapicha hao kumi, wawili kutoka kila nchi.
Tanzania
inawakilishwa na Mpigapicha Mwandamizi wa Magazeti na Habari za
Mtandao, Mroki Mroki, Mwasisi na Mhariri Mkuu wa FATHER KIDEVU BLOG
pamoja na Mwandshi wa Kampuni ya Mwanachi Comunication mjini Arusha,
Filbert Rweyemamu.
Tayari
wapigapicha hao wa Habari wapo mkoani Arusha wakiwasubiri wenzao wa
Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kuwasili kwa kuanza mafunzo hayo.
Mkufunzi
wa mafunzo hayo ni Balozi wa Heshima wa Utalii nchini Kenya na
Mwenyekiti wa mfuko wa 50 Treasures of Kenya, Hartmut Fiebig.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!