MABINGWA
watetezi wa Kombe la kagame leo imefunzi kucheza nusu fainali ya kombe
la Kagame kwa kuilaza Mafunzo ya Zanzibar kwa mikwaju 5-3 ya penati
baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare 1-1.
Mafunzo
wanakila namna ya kujutia mchezo wa leo ambao Said Bahanuzi amefikisha
goli la 7 baada ya kufunga magoli mawili moja la kuisawazishia Yanga na
lapili katika matuta.
Mafunzo
ilikosa penati moja kupitia mchezaji wake Saidi Shaban jambo
lililoigharimu timu hiyo iliyoonesha kiwango cha hali yajuu katoka soka
hii leo.
Aidha
Yanga ambayo awali ilikuwa ikifurahia kupita kilaini katika mchezo
waleo nayo itabidi kujifua kikamilifu katika mchezo wake wa nusu fainali
hasa kwa washambuliaji wake ambao mara kadhaa walikuwa wakikosa magoli
hususani Hamis Kiiza.
Katika
dakika 90 za mchezo Mafunzo kutoka Zanzibar , ili ivimbishia msuli
Mabingwa wa watetezi wa Kombe la Kagame, Yanga ya Dar es Salaam kwa
kumaliza nao mchezo kwa sare ya 1-1, katika mchezo war obo fainali ya
pili ya Michuano ya CECAFA Kagame CUP 2012.
Mafunzo
na Yanga zote kutoka Tanzania bara na Visiwani zimechuana katika mchezo
wa wa pili wa robo fainali ya Kombe la Kagame 2012 katika uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Timu
ya Mavunzo imeonesha kiwango kikubwa cha soka safi huku wakifanya
mashambulizi ya mara kwa katika lango la Yanga ambao wanapewa nafasi
kubwa ya kushinda mchezo wao wa leo.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!