StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

July 22, 2012

GREDA LAGONGA MWENDESHA PIKIPIKI MJINI MUSOMA JANA JIONI

Tweeted this Like this, be the first of your Friends
 
Ajali mbaya iliyohusisha Greda na Bodaboda imetokea alasiri hii mjini Musoma katika makutano ya Barabara ya Shabani na Bus Stop. Ajali hiyo imepelekea abiria (mwanamke pichani) aliyekuwa amepakiwa katika pikipiki hiyo kujeruhiwa vibaya maeneo ya tumbo na paja  baada ya kuburutwa na mashine hiyo ya kutengenezea barabara.

Hata hivyo limetokea gari la shirika la umeme Tanesco na kumchukua majeruhi huyo na kumkimbiza katika hospitali ya Mkoa wa Mara. Mpaka mwandishi wetu anaondoka eneo la tukio kulikuwa na sintofahamu ya ni wapi dereva wa pikipiki na greda hilo walipoelekea kwani mashuhuda wa tukio hilo wanasema dereva wa pikipiki alikimbia punde tu ajali ilipotokea.
 Pikipiki iliyopata ajali hiyo
Umati wa watu uliofurika eneo la tukio

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat