Diwani wa kata ya Buhemba Boniphace Masero akifafanua jambo kwa waandishi wa habari
Augustine Mgendi, BUHEMBA
WANANCHI
vijiji Vitatu wanaozungukwa na Mgodi wa Buhemba wilaya ya Butiama
mkoani Mara wanakusudia kuishitaki Serikali ya Tanzania katika Taasisi
za Umoja waMataifa zinazohusika na haki za binadamu ikiwa ni shinikizo
la kulipwa fidia ya shilingi Bilioni 30.
Mbali
na kusudio hilo la kuelekea umoja wa Mataifalakini pia wananchi hao
wamesema kuwa wanakusudia kumuona Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania
Jakaya Kikwete kumueleza madhara yaliyosababishwa na Mgodihuo ambao
ulidaiwa kumilikiwa na Serikali kupitia Kampuni ya Meremeta.
Wananchi
hao kutoka vijiji vyaTarani,Biatika na Magunga huku wakiomba Wabunge
kuungana na kutoipitisha Bajetiya Wizara ya Nishati na Madini had hapo
Serikali itakapo wafidia.
Akiongeana
waandishi habari katika eneo hilo la Buhemba,Diwani wa kata ya
BuhembaBoniphace Masero amesema kuwa Mgodi huo umeachia athari kubwa
kutokana namachimbo yaliyoachwa kuleta athari kubwa huku Ardhi yao ikiwa
haina rutuba kutokanana Kemikali zilizomwagwa katika eneo hilo
Amesema
athari zingine zilizoletwa na Mgodi huo nipamoja na Shule iliyokuwa
katika eneo hilo kubomolewa lakini walishindwakuijenga kama walivyokuwa
wameahidi wahuska hao wa mgodi huku miundombinu yabarabara nao ikiwa
haifai kutumika.
“Huu
Mgodi umetuachia madhara makubwa sana maanaMashimo hayakufukiwa,Milima
inaleta uchafuzi wa Mazingira,shule iliyokuwaimejengwa hapa
ilibomolewa,Nyumba zikabomoka kutokana na Baruti za mgodi,katikahili
sisi tunakusudia kumuona Rais ili tumueleze haya Manyanyaso
tunayoyapata”alisema diwani huyo
Diwani
Masero ameongeza kuwa athari nyingine nipamoja na baadhi nyumba za
wakazi wa eneo hilo kubomoka kutokana na barutizilizokuwa zikipigwa
katika Mgodi huo lakini mpaka sasa hawajalipwa fidia nahivyo wanawaomba
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakutoipitisha Bajeti
ya wizara ya Nishati na Madini mpaka walipwe fidia yao
Aidha
Pasta wa Kanisa la Anglikana SamweliNyakarungu alisema kuwa mgodi huo
wa Buhemba ulikuwa ni Mgodi wa kitapeliambapo wahusika hao wamechuma
raslimali za Taifa na kushindwa kufanya shughuliza Maendeleo katika
Jamii.
Pasta
Nyakarungu alisema kuwa mbali na wawekezajihao wa Kitapeli kuiba mali
ya Watanzania lakini pia wamesababisha madharamakubwa kwa jamii ya
Buhemba kwa kushindwa kujenga miundombinu ya barabara,kujengashule kama
inavyotakiwa.
Kutoka
na adha hiyo Pasta huyo alisema kuwa Serikaliimeshindwa kuwajali
wananchi wake na hivyo wanawaomba Wabunge wa Bunge laJamhuri ya Muungano
kutoipitisha Wizara ya nishati na Madini mpaka hapowananchi wa eneo
hilo watakapopata fidia yao.
“Hawa wawekezajimimi naona hawakuja hapa kwa lengo la kumsaidia mtu wa
Buhemba huu Mgodi naonaulikuwa wa Kitapeli kabisa,wamechuma raslimali za
Taifa na kushindwa kumsaidiamtu anayezungukwa na mgodi na hata
kurekebisha miundombinu huska na hiiinaonyesha jinsi Serikali isivyojali
wananchi wake” alisema Pasta Nyakarungu
Naye
Mwalimu mstaafu Sita Nyamhanga na bi HadjaYasini walisema kuwa mgodi
huo umewaachia matatizo makubwa ikilinganishwawalivyokuwa wameahidiwa
wakati wanaanza uchimbaji katika mgodi huo.
“Tunavyojuani
kwamba wawekezaji wanapowekeza eneo lolote lazima watu wanaozungukwa
naMgodi ule wanufaike lakini hapa Buhemba sisi wananchi ndiyo tumepat
tabu kabisakwani mpaka sasa hatuna shule,barabara inayopitika muda
wote,eneo letu limebakiJangwa huku wakina mama wanapata tabu kutafuta
maji kutokana na vyanzo vingivya maji kuchafuliwa na mgodi” alisema
Mwalimu mstaafu huyo.
Kwa
upande wake Bi Hadja Yasini alisema kuwawanapata tabu hata kutafuta
kuni kutokana na eneo kubwa la Buhemba kubakiJangwa tofauti na
ilivyokuwa hapo awali.
Kulingana
na adha hiyo Bi Hadja alisema kuwa nivyema Waziri mwenye dhama huska
akawasaidia watu wa Buhemba ili waweze kupatafidia zao kutokana na
madhara waliyoyapata kutokana na mgodi huo.
Mgodi
wa Buhemba ambao ulianza kuchimbwa mwaka 2002ni moja ya mgodi ambao
ulikuwa ni mkubwa hapa nchini ukielezwa kumilikiwa naSerikali na
kufungwa mwaka 2006 huku ukiacha eneo hilo la Buhemba kupotezarutuba
yake
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!