Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
OFISI ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inatarajia
kufanya usaili wa watumishi 18,105 kujaza nafasi zilizo wazi katika
Utumishi wa Umma.Nafasi hizi zipo katika Wizara na Idara zinazojitegemea
ambazo ni 7,896, Sekretarieti za Mikoa nafasi 1,339, Halmashauri za
Wilaya nafasi 7,892 pamoja na Taasisi na Wakala wa Serikali nafasi 978.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais – Manejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina
Kombani alisema jana Bungeni kuwa nafasi hizo ni nje ya nafasi
zinazohusu Wizara ya Kilimo, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Elimu, Afya
na Mifugo.
“Mpango wa mwaka 2012/2013, Sekretarieti ya Ajira
inatarajia kutumia jumla ya Sh2.5 bilioni kwa ajili ya Matumizi ya
Kawaida,” alisema Kombani.
Kwa upande wake, Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Umma inatarajia kutumia Sh7.9 bilioni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida.
Alisema
miongoni mwa kazi zilizopangwa kutekelezwa na tume hiyo kutoa uamuzi wa
rufaa na malalamiko kadri yatakavyopokelewa, kufanya ukaguzi wa
rasilimali watu kwa waajiri, mamlaka za ajira na nidhamu na kufuatilia
uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu za usimamizi wa Rasilimali
watu katika Utumishi wa Umma.
Alizitaja kazi nyingine kuwa ni
kuendelea kuelimisha wadau kuhusu shughuli za tume kupitia njia
mbalimbali kama vile vyombo vya habari, maonyesho na ziara.
Kombani
pia alizungumzia Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma
kwamba bodi hiyo itaendelea kufanya tafiti juu ya hali ya mishahara
ikilinganishwa na hali halisi ya uchumi ili kutoa mapendekezo
yanayohusiana na marekebisho ya mishahara na maslahi.
“Bodi hii itaendelea kukusanya, kulinganisha na kuchambua
taarifa
zinazohusiana na masuala ya gharama za maisha, nyumba na vigezo vingine
vinavyohusiana na malipo ya posho na maslahi mengine,” alisema Kombani
na kuongeza:
“Kutoa mapendekezo juu ya kiwango cha mishahara,
posho na maslahi kwa ajili ya mihimili mitatu ya Dola, kutoa ushauri
kuhusu misingi ya miundo ya mishahara katika Utumishi wa Umma na
kushauriana na Taasisi husika za Serikali juu ya bajeti ya kila mwaka
kwa ajili ya malipo ya mishahara na maslahi ya Watumishi wa Umma”.
July 3, 2012
Maelfu kuajiriwa kuziba nafasi zilizo wazi Serikalini
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget