TIMU ya vijana ya Mkoa wa Morogoro, chini ya umri wa miaka 17, jana ilifanikiwa kuibuka na ubingwa wa michuano ya Copa Coca Cola kwa bao 1-0 dhidi ya Mwanza kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Moro ambayo ilifika fainali baada ya kuifunga Temeke mabao 3-1, ilipata bao lake kupitia kwa Salum Ramadhani katika dakika ya 36.
Mara baada ya mpira kumalizika, vijana wa Morogoro walianza kucheza muziki baada ya kupigiwa wimbo wa Dar Mpaka Moro ulioimbwa na TMK Wanaume Family.
Kocha wa Morogoro, Mecky Mexime alisema: “Nimefurahishwa na ubingwa licha ya kuwa tulianza kwa kusuasua.”
Aidha katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu, Temeke ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanga, mfungaji akiwa Lean Kibingo katika dakika ya 65 na 82.
Mfungaji bora kwenye michuano hiyo ni Mtalemwa Abogas, ambaye amefanikiwa kufunga mabao kumi kwenye kikosi chake cha Moro, timu yenye nidhamu ni Tanga, wakati kocha bora ni Mohammed Kampira aliyekuwa akiifundisha Tanga.
www.globalpublishers.info
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!