Meneja
Mauzo wa Airtel Kanda ya Pwani, Amina Keita (kushoto) akitoa zawadi ya
simu kwa mmoja wa wakazi wa Mtwara, Nasra Salehe wakati wa uzinduzi wa
huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara jana.
Tukio hilo liliambatana na burudani kutoka kwa wasanii chipukizi wa
mkoani humo na baadhi ya wasanii maarufu kutoka katika Jiji la Dar es
Salaam ambako waliohudhuria walielezwa jinsi ya kujiunga na faida mbalimbali zinazopatikana katika huduma ya Supa 5.
Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane
Matinde akihutubia wakati akizindua huduma ya Supa 5 ya Airtel katika
Uwanja wa Mashujaa Mkoani Mtwara jana.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya
kutoka THT, Mwasiti Almasi akikonga nyoyo za wakazi wa Mtwara
waliohudhuria uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa
Mashujaa Mkoani Mtwara jana.
Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania,
Jane Matinde (kulia) akitoa zawadi ya simu kwa Jamimu Mohamed baada ya
kuibuka mshindi kwa kutoa maelezo sahihi ya jinsi ya kujiunga na faida
za huduma ya Supa 5 ya Airtel wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika
Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara jana.
Msanii mkali wa miondoko ya bongo
flava, Juma Kassim Nature ‘Sir Nature’ kutoka kundi la Wanaume Halisi,
akifanya vitu vyake wakati wa uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya Airtel
katika Uwanja wa Mashujaa Mkoani Mtwara jana.
Mwanamuziki wa miondoko ya hip hop,
Ibrahim Mussa anayekwenda kwa jina la ‘Roma Mkatoliki’ akighani moja ya
shairi la wimbo wake uliompatia umaarufu wa ‘Pastor’ katika uzinduzi wa
huduma ya Supa 5 ya Airtel katika Uwanja wa Mashujaa Mkoani Mtwara jana.
Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa
Mtwara na viunga vyake wakifuatilia uzinduzi wa huduma ya Supa 5 ya
Airtel katika Uwanja wa Mashujaa mjini humo jana.
Mabinti wa Mtwara wakichuana ili
kumpata mshindi wa kusakata ‘Kiduku’ ambapo mshindi wake, Nasra Salehe
(kushoto) alijishindia simu katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Supa 5
ya Airtel Mkoani Mtwara.