Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Hapo zamani watu walikuwa wanamuona mtoa roho (Izraeli) anapokuja kuchukua roho zao.
Siku moja alienda kutoa roho ya jamaa mmoja aliyekuwa tapeli maarufu katika nchi ya misri. Mtoa roho alipofika akamwambia
Mtoa roho: kwa mujibu wa listi yangu hapa inaonekana kuwa leo ndio siku yako ya kufa
Tapeli: enheeeee! nashukuru kweli maana nilikuwa naisubiri hiyo siku kwa hamu na nilikuwa nashangaa kwa nini unachelewa kuja
Mtoa roho: basi mshukuru mungu wako nimefika
Tapeli: Kwa furaha niliyo nayo naomba nikununulie hata soda au maziwa unywe halafu tuendelee na kutoa roho yangu
Mtoa roho akakubali na kukaribishwa soda. Kumbe yule tapeli akamtilia kilevi kikali katika soda. kisha mtoa roho alipolewa na kulala akaichukua ile listi ya mtoa roho halafu akaliweka jina lake chini kabisa tokea kule juu.
Baada ya muda yule mtoa roho akaamka baada ya kilevi kile kumuisha na kusema
Mtoa roho: Aisee kutokana na ukarimu uliouonyesha wa kunikaribisha kinywaji basi nitakupendelea ili usife leo
Tapeli: Kweli!?
Mtoa roho: ndio, nilipokuwa nimelala niliongea na mungu na kumuomba ruhusa kuwa nisianzie juu kwenda chini katika orodha yangu badala yake nianzie chini kwenda juu ili uwe wa mwisho na mungu amenikubalia hivyo naomba listi yangu katika begi nijue nani wa chini
October 16, 2012
VUNJA MBAVU: MAHOJIANO YA MTOA ROHO (IZRAELI) NA TAPELI MMOJA
Millionfortune.com
VUNJA MBAVU
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!