Bingwa mtetezi wa mchezo wa Tennis aliyeshinda medali ya dhahabu wakati wa mashindano ya Olimpiki mjini Beijing Rafal Nadal amejiondoa kutoka London 2012, kwa hoja kua hali yake haitomuezesha kushiriki.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anaumwa goti na hatoweza kutetea taji lake.
Nadal alisema wakati akitangaza hayo “nimejikuta kuwa sitoweza kushindana katika hali hii,” akiongezea kua . “nina masikitiko makubwa ya kutoshiriki.”
Mshindi huyo wa mashindano makubwa mara 11 alitazamiwa kuiongoza Timu ya Uhispania na kuibeba bendera ya Taifa kwenye sherehe ya ufunguzi mjini London.