Askari
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakitoa heshima kwenye mnara wa
kumbukumbu ya Mashujaa katika viwanja vya mnazi mmoja leo ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya
mashujaa.
Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (katikati) akiongea na
waandishi wa habari Katika viwanja vya Mnazi mmoja leo jijini Dar es
Salaam kueleza namna mkoa ulivyojipanga kufanikisha sherehe za
maadhimisho ya siku ya mashujaa itakayofanyika kitaifa tarehe 25, Julai
2012 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Kiongozi
wa mabalozi wanchi za Afrika wanaoishi nchini Tanzania Balozi Ibrahim
Mukubi kutoka Uganda akiweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu
ya mashujaa leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya
sherehe ya siku ya mashujaa itakayofanyika tarehe 25, Julai 2012.
Askari
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) watakaoshiriki kwenye gwaride
wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa wakiendelea na mazoezi katika
viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO
---
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Wananchi
wa mkoa wa Dar es salaam wameombwa kujitokeza kwa wingi wakati wa
sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa itakayofanyika
kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja tarehe 25 Julai 2012 jijini Dar
es salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam , Mkuu wa mkoa wa Dar
es salaam Saidi Meck Sadiki amesema maandalizi ya maadhimisho hayo
yamekamilika na kufafanua kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo atakuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
Amesema
katika maadhimisho hayo kwa upande wa mkoa wa Dar es salaam baadhi ya
barabara zitafungwa ikiwemo barabara ya Nyerere, Uhuru na Bibi Titi
Mohamed ili kuhakikisha usalama kwa wale wote watakaohudhuria
maadhimisho hayo na kuongeza kuwa katika kuboresha maadhimisho hayo
kamati ya maadhimisho itaweka luninga katika maeneo yote muhimu ili
kuwawezesha wananchi kuona yanayotendeka wakati wa maadhimisho hayo.
Aidha
Bw. Meck Sadiki amesema kuwa maadhimisho hayo ni kumbukumbu muhimu
katika historia ya Tanzania kwa kuwaenzi mashujaa waliojitoa muhanga
katika jitihada za kuikomboa na kuilinda Tanzania.
“
Maadhimisho haya ni kumbukumbu muhimu sana katika historia ya nchi yetu
kwani tunawaenzi mashujaa wetu waliojitoa muhanga katika jitihada za
kuikomboa, kuilinda na kudumisha amani na utulivu wan chi yetu”
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!