Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
TANZANIA imependa kwa nafasi 12 kwenye orodha ya viwango vya ubora vya
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) vilivyotolewa jana na
hivi sasa inashika nafasi ya 127.
Kwa mujibu wa viwango vya Fifa,
mwezi uliopita Tanzania ilikuwa ikishika nafasi ya 139,sasa imepanda
baada ya kufikisha pointi 253 tofauti na mwezi uliopita ilikuwa na
pointi 214.
Tanzania imepanda baada ya mwezi uliopita kucheza na
Ivory Coast na kufungwa mabao 2-0, pia ilicheza na Gambia na kushinda
2-1 kabla haijatoka sare ya 1-1 na Msumbiji.
Mechi kati ya
Tanzania dhidi ya Msumbiji ilikuwa ya kuwania kufuzu kushiriki Fainali
za Kombe la Mataifa ya Afrika 2013 na mechi dhidi ya Ivory Coast pamoja
na mechi dhidi ya Gambia zilikuwa ni mechi za kuwania kufuzu Fainali za
Kombe la Dunia 2014.
Matokeo ya sare iliyopata Tanzania
ilipocheza dhidi ya Msumbiji mjini Maputo, yalisababisha kupigwa penalti
na hivyo Tanzania kutolewa katika mashindano ya kuwania kufuzu
kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika 2013.
Katika kufuzu
Fainali za Kombe la Dunia hivi sasa Tanzania inashika nafasi ya pili
katika kundi lake ikiwa imezidiwa na Ivory Coast ikizitangulia Morocco
na Gambia.
Uganda imeendelea kuongoza Ukanda wa Afrika Mashariki
katika nafasi ya 85 ikipanda nafasi tisa ikifuatiwa na Kenya nafasi ya
125 kisha Rwanda nafasi ya 126.
Nchi ya Burundi katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki yenyewe inashika nafasi ya 136.
Huu
ni mwanzo mzuri kwa kocha mpya wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania
(Taifa Stars) ambapo ameanza kazi na kuipandisha Tanzania katika viwango
hivyo vya Fifa.
Viwango hivi vya Fifa ni muhimu katika upangaji
wa ratiba za mechi, ambapo nchi zinazoshika nafasi ya juu hupewa nafasi
mbili za juu katika kila kundi la timu nne na zile zinazoshika nafasi za
chini hupewa nafasi mbili za chini.
Kutokana na Tanzania kuwa
katika nafasi za chini katika viwango hivi vya Fifa imejikuta kila mara
ikipangiwa timu ngumu kwenye mashindano na hivyo kutolewa katika hatua
za awali.
Ivory Coast inashika nafasi ya 16 katika viwango vya Fifa
na kuendelea kuongoza kwa upande wa Afrika, ambapo pia ilikuwa katika
nafasi hiyohiyo kwa viwango mwezi uliopita.
Hispania ambao ni mabingwa wa Ulaya na Dunia, ndiyo wanaoendelea kuongoza kwa ubora wakishika nafasi ya kwanza.
July 5, 2012
Tanzania yapanda kwa nafasi 12 Fifa
Millionfortune.com
MICHEZO
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget