Ukuaji wa uchumi wa China umepungua na kufikia kiwango cha
chini katika muda wa miaka mitatu katika robo ya hivi sasa ya
mwaka huu, wakati mauazo ya nje na uwezo wa watumiaji
ukidhoofika. Data zilizoripotiwa leo zinaonyesha kuwa uchumi huo
wa pili kwa ukubwa duniani umeongezeka kwa asimilia 7.6 katika
miezi mitatu iliyomalizikia Juni, ikiwa ni chini kutoka asilimia 8.1
katika robo iliyopita ya mwaka huu. Huo ni ukuaji wa taratibu
mno tangu robo ya kwanza ya mwaka 2009 wakati mzozo wa
kifedha duniani ulipokuwa ukiendelea. Ongezeko la bidhaa
zinazouzwa nje limepungua taratibu huku kukiwa na matatizo ya
mahitaji duniani na uwezo wa wawatumiaji nchini China
umedhoofika. Serikali imepunguza riba mara mbili tangu
mwanzoni mwa mwezi Juni na kuanzisha hatua kadhaa za
kuchochea ukuaji wa uchumi. Wadadisi wa masuala ya kiuchumi
wanatarajia ukuaji wa uchumi kurejea tena katika hali yake ya
kawaida katika sehemu ya pili ya mwaka huu lakini mdororo
wa uchumi unaongeza kitisho cha upotevu wa nafasi za kazi
pamoja na kuleta wasiwasi wa kisiasa.
July 13, 2012
Uchumi wa China wapungua kasi ya ukuaji
Millionfortune.com
UCHUMI
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!