NAIBU
Spika, Job Ndugai Alhamisi Julai 12, 2012 bungeni alitangaza kuwa
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA) atafikishwa kwenye Kamati ya
Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge baada ya kushindwa kutoa ushaidi wa
kuhusika kwa mbunge wa Iramba Maghaaribi (CCM), Mwigulu Nchemba, katika
wizi wa Fedha za Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).
Awali
Mwigulu aliomba mwogozo nakusema wiki iliyopita Mnyika alimhusisha na
wizi wa EPA uliofanyika wakati yeye (Mwigulu) akiwa chuoni na kiti cha
Spika kilimpa Mnyika siku saba kutoa ushahidi dhidi ya tuhuma hizo.
Akitoa
mwongozo wake, Ndugai alisema Mnyika alitakiwa apeleke ushahidi wa
tuhuma hizo lakini amepeleka maandishi ya utangulizi ila si ushahidi.
“Kwa
kuwa siku saba zimepita sasa mwongozo wangu ni…suala hili sasa
ninalipeleka katika Kamati ya Haki Maadili na Madaraka ya Bunge,
ataandikiwa barua na kamati hiyo ndiyo itakayoshughulikia ushahidi huo,”
alisema.
Mapema
katika madai yake Mwigulu alisema siku saba alizopewa Mnyika
kuthibitisha tuhuma hizo ambazo zililenga kumvunjia heshima kwa chama
chake, Watanzania na wapiga kura wake.
“Bunge
lako linajua na Watanzania wanajua kwamba wakati tuhuma za EPA
zinatokea mimi nilikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu, nilikuwa bado
sijaajiriwa BoT,” alisema.
Baada
ya kauli hiyo Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani, Tundu Lissu, aliomba
kiti cha spika (Ndugai), kimwelekeze Nchemba matumizi halali ya mwongozo
wa Spika kwa mujibu wa kanuni 68(7), inahusu jambo ambalo limetokea
mapema kikao kinachoendelea.
“Sasa
mheshimiwa Spika hili jambo ambalo mbunge analizungumzia lilitokea wiki
iliyopita, pili kuna maelekezo tayari yaliyotolewa na kiti chako kwamba
mheshimiwa Mnyika alete maelezo ya uthibitisho kwa kiti chako na
maelekezo yalishatolewa ningefikiri ni jambo la busara kusubiri ofisi
yako iseme kama imepata majibu ama haijapata sasa anachotaka huyu
anataka mwongozo wa namna gani?” alihoji.
Pamoja
na wapenzi wa CHADEMA na MNYIKA kuhoji namna mwongozo wa Ndugai kwa
Mwigulu ulivyo shugulikiwa, kwa madai kwamba jambo hilo limetolewa
ufafanuzi mapema wakati kuna viporo vingi vya miongozo ya wabunge
havijatolewa uamuzi hoja hiyo haitooshi kumuokoa Myika.
Baadhia
ya miongozo iliyokaa kwa muda mrefu ni pamoja na madai ya aliyekuwa
mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, kudai kuwa Waziri Mkuu
alilidanganya Bunge kuhusu vurugu za Arusha Januari 5 mwaka jana.
Hadi
Lema anavuliwa ubunge na Mahakama Aprili mwaka huu, suala hilo lilikuwa
halijatolewa uamuzi, huku madai ya mbunge wa Kigoma Kusini
(NCCR-Mageuzi), David Kafuli ya Julai mwaka jana kuwa baadhi ya wabunge
wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa waliomba rushwa kwenye
halmashauri nayo hadi leo hayajatolea uamuzi.
Lakini pia vipo viporo vya Tundu Lissu dhidi ya William Ngeleja, Kabwe Zitto dhidi ya Mustafa Mkullo na wengine wengi.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!