Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Watu wawili wamefariki dunia na
wengine 24 kujeruhiwa baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiria kutoka
Moshi kwenda Arusha mjini kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa
limebeba mchanga aina ya Fuso.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alithibitisha
kutokea kwa ajali hiyo maeneo ya Tengeru wilayani Arumeru jana mchana.
Alisema waliofariki dunia ni dereva na utingo wa basi dogo ambao majina yao hayakupatikana mara moja.
Kamanda Sabas alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi dogo
kujaribu kulipita gari lingine na wakati akifanya hivyo, lilitokea lori
hilo na kugongana.
Alisema wakati ajali hiyo ikitokea lori hilo liliparamia tena gari dogo aina ya Toyota Chaser.
Alisema majerusi sita wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru
na 12 wamelazwa kwenye zahanati ya Tengeru na wengine wanne walitibiwa
na kuruhusiwa kuondoka.
CHANZO: NIPASHE
August 7, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!