WAKATI
taarifa za kurejea nchini kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk
Steven Ulimboka zinasemwa bila wausika kuthibitisha viongozi wa Jumuiya
hiyo na Umoja wa Madaktari Tanzania (MAT), wanatarajia kukutana Jumanne
Augosti 7, 2012 kujadili tukio zima lililomkumba kiongozi huyo. Baada ya
kikao hicho, madaktari hao watakutana na familia yake na kisha
kumuuliza Dk Ulimboka kama angependa kilichomtokea kiwekwe wazi kwa
jamii.
DR. ULIMBOKA BAADA YA KUOKOTWA MSITU WA PANDE
Dk
Ulimboka ambaye alikuwa anaratibu mgomo wa madaktari uliokuwa
ukiendelea nchi nzima, alitekwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia
Jumatato ya Juni 27 mwaka huu na kupelekwa katika msitu wa Pande, nje
kidogo ya Jiji a Dar es Salaam, ambako aliteswa na kujeruhiwa vibaya.
Katika tukio hilo daktari huyo aling’olewa meno mawili na kucha za mkono
mmoja na baadaye kulazwa katika Kitengo cha Wagonjwa Wanaohitaji
Uangalizi Maalum (ICU) katika Taasisi ya Mifupa (MOI).
Baada
ya hali yake kuzidi kuwa mbaya Juni 30 mwaka huu, alisafirishwa kwenda
Afrika ya Kusini kwa ajili ya vipimo na matibabu. Kusafirishwa kwake
kulifuatia taarifa ya jopo la madaktari lililokuwa linamhudumia kutoa
taarifa kwa madaktari bingwa kuhusu mabadiliko ya afya yake. Taarifa za
kurejea kwa Dk Ulimboka zimezagaa katika mitaa mbalimbali jijini Dar es
Salaam, huku baadhi ya watu wakizijadili katika mitandao ya kijamii.
Katibu
wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Edwin Chitage, alisema kati ya
Agosti 7 au 8, 2012 viongozi mbalimbali wa MAT na Jumuiya ya Madaktari,
watakutana kujadili suala la kiongozi huyo. “Ndani ya siku mbili hizi
(Agosti 7 au 8) viongozi tutakutana na kujadili ripoti ya matibabu ya Dk
Ulimboka na tutajadili kama tuvieleze vyombo vya habari ama laa,”
alisema Dk Chitange.
Hata
hivyo Dk Chitange alisema hatua hiyo itategemea na kauli ya familia ya
Dk Ulimboka na yeye mwenyewe (Dk ULimboka) kwa kuwa na wao pia
watashirikishwa.
“Dk
Ulimboka na familia yake tutawashirikisha katika mambo ambayo
tutayajadili,” alisema Dk Chitage. Alipoulizwa kama kiongozi huyo wa
madaktari sasa anaweza kufanya shughuli zake kama awali, alisema hana
uhakika kwa kuwa hana taarifa za ndani zaidi .