StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

August 23, 2012

AJALI YA ALIYEKUFA KWA KUKANYAGWA KICHWA NA LORI LEO

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Baadhi ya wananchi wakiwa wanaangalia mwili wa marehemu ambaye amepoteza maisha papo hapo mara baada ya kugongwa na lori na kukanyagwa kichwa na hatimaye kupelekea kichwa kupasuka na ubongo kumwagika chini leo majira ya saa tisa mchana eneo la ilala boma



Mwili wa marehemu ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja ukiwa umefunikwa na kanga huku pembeni vipande vya ubongo wake vikiwa pembeni mara baada ya kugongwa na lori na kukanyangwa kichwa na kupelekea kichwa kupasuka na ubongo wote kumwagika chini leo majira ya saa tisa mchana eneo la Ilala Boma. Kijana huyu anasadikiwa kuwa ni mwanafunzi wa Darasa la Saba katika shule ya Msingi Msimbazi.


Askari wa Usalama barabarani akisaidiana na baadhi ya wananchi kuubeba mwili wa marehemu ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja ili kuupakia katika gari dogo tayari kuupeleka hospitali ya Amana.Kijana huyu anakadiriwa kuwa ni mwanafunzi wa Darasa la Saba wa Shule ya Msingi Msimbazi.


 Baadhi ya wananchi wakiutazama mwili wa marehemu ambaye amegongwa na gari na kupelekea kupasuka kichwa na kupoteza maisha papo hapo.


Mwili wa marehemu ukifunikwa vizuri kwaajili ya kupelekwa hospitali ya amana.Pembeni ya mwili wa marehemu ni vipande vya ubongo mara baada ya kukanyangwa na lori


Kijana wa kiume ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja amepoteza maisha mara baada ya kugongwa na lori leo majira ya Saa tisa Mchana eneo la Ilala Boma karibia na Ofisi ya Mkuu Wa Mkoa wa Dar Es salaam. Mara baada ya kugongwa na lori, lori hilo liliweza kukimbia na halikujulikana ni wapi limeelekea na namba za gari hizo hazikuweza kupatikana mara moja.

Kijana huyu anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 14 ambaye pia shuhuda wa ajali hii ameueleza mtandao wetu kuwa ni mwanafunzi wa shule ya msingi Msimbazi Center kutokana na sare za shule alizokuwa amevaa.

Shuhuda wa Ajali hii ambaye hakupenda jina lake kuchorwa na mtandao wetu amesema kuwa Wakati kijana huyo anavuka barabara lori lililomgonga lilikuwa linatokea maeneo ya buguruni na kumgonga kijana huyo. Mara baada ya kumgonga lilimkanyaga kichwani " Lilianza tairi la mbele kumkanyaga kichwa halafu likafuatia na tairi la nyuma ambapo lilipelekea kichwa kupasuka vibaya na hatimaye ubongo kusambaa barabarani kama ambavyo unao hapo chini na hatimaye lori hilo kukimbia" alisema shuhuda huyo.

Na hivi ndivyo shuhuda wetu alivyojibu " Kiukweli Nilishindwa kuandika au kunakili namba ya usajili wa lori kwasababu kwanza niliposikia kitu kizito kimegongwa na hilo lori nilijua ni mtu wa bodaboda wakati naangalia vizuri nikaona ni kijana mdogo ndiye amegongwa na lori likimkanyaga kichwa likiwa katika harakati ya kukimbia hapo nilishindwa kuandika chochote kwasababu nilipigwa na butwaa na kubaki kama bumbuwazi na mwili kushikwa na ganzi mara baada ya kuona ubongo vipande vya ubongo chini" alisema shuhuda wetu

Mpaka chanzo chetu kinaondoka eneo la tukio lori lililomgonga halikuweza kupatikana wala kujulikana lilipoelekea na jina la kijana aliyepoteza uhai papo hapo nalo halikuweza kupatikana

1 comments:

zennat khamis said...

huyo mtoto aliyegongwa anaitwa ABDULKARIM MOHAMED MDEE,anamiaka 11 wmanafunz wa darasa la 4 katika shule ya msingi ILALA BOMA....baada ya kumgonga dereva wa roli alikimbia na kujisalimisha polisi na kesi yake imetajwa tarehe 3-9-2012 ambapo amehukumiwa kulipa faini 50000TSH au jela miezi 6

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat