Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Watu kumi na saba wamekufa na wengine 78 kujeruhiwa wilayani Sikonge katika Mkoa wa Tabora baada ya basi la Sabena aina ya Scania lenye namba T570 AAM kupata ajali na kupinduka.
Basi hilo lilikuwa likitoka Tabora kwenda Mbeya.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kitunda wilayani Sikonge umbali wa kilometa 200 kusini mwa mji wa Tabora.
Miongoni wa watu waliokufa ni watoto watano, wanawake sita na wanaume sita na hadi leo mchana, miili ya watu saba ilikuwa imetambuliwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Antony Ruta, alisema basi hilo lilikuwa limejaa kupita kiasi kwani inaonekana lilikuwa na abiria zaidi ya 100.
KAMANDA WAPOLISI MKOA WA TABORA ACP ANTON RUTTA AKITOA MAELEZO KWENYE VYOMBO YA VYA HABARI KWENYE ENEO LA TUKIO
MMMOJA WA MAJERUHI WA AJALI HIYO AKIZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI
Hata hivyo, hadi kufikia leo mchana, miili ya watu saba ilikuwa
imetambuliwa na baadhi ya ndugu, ukiwemo wa askari Polisi Konstebo
Kheri, wa Kituo Kikuu cha Polisi cha mjini Tabora.
Marehemu wengine
waliotambuliwa ni Vitus Tulumanye, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Augustine (SAUT), tawi la Tabora na Farah Inga raia wa
Zimbabwe aliyekuwa akifanyakazi Tabora.
Wengine waliotambuliwa ni
Ikamba Thadeo, Damalu Goma, Beatrice Kalinga ambaye ni mwalimu wa shule
ya msingi Igoko wilayani Uyui mkoani Tabora na Madirisha ambaye ni
mwalimu wa shule ya msingi iliyoko wilaya Mpya ya Kaliua.
Mwalimu
Madirisha anadaiwa kufuatana na watoto wanne na mkewe ambaye bado
hajatambuliwa najuhudi zinaendelea za kubaini familia ya mwalimu huyo.
Kwa
mujibu wa maelezo yaliyotolewa na aliyenusrika katika ajali hiyo kwa mwakilishi wa
basi hilo mkoani Tabaro, Shaaban Mnyema, chanzo cha ajali hiyo ni lori
aina ya Fuso lililokuwa limeegeshwa katika kona. Aidha Alidai kuwa kutokana na mwendo wa kasi lililokuwa nalo, dereva wa
basi hilo alipojaribu kulikwepa fuso hilo ndipo 'Stearing Road' ilipokatika na kusababisha gari kuacha
njia na kupinduka.
Dereva wa basi hilo Ali Nassoro, ambaye alitoroa baada ya
kutoa taarifa za ajali na maelezo hayo kwa njia ya simu, alisema ajali
hiyo ilitokea jana saa 6.30 mchana katika eneo ambalo halina mawasiliano
ya simu za mkononi.
Nassoro alisema hata katika kijiji cha Kitunda
kulikuwa hakuna mawasiliano na hivyo kumlazimi kumtuma mtu kwenda
Sikonge kutoa taarifa za ajali hiyo.
Baadhi ya majeruhi
waliotambuliwa ni Grace Mbunga, Kayungilo Nsungu, Zena Shigela, Ndisi
Ngosha, Kulwa Kija, Feni Salum, Shinje Kayogole na Emmanuel Charles.
August 9, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!