StatsCrop - Free website analyzer!

Ads 468x60px

AddToAny

Lorem

Social Icons

October 4, 2012

MAAFISA WA VYOMBO VYA ULINZI USALAMA WAFANYA OPARESHENI KUIKAGUA MELI MPYA YA AZAM SEALINK-1.

Tweeted this Like this, be the first of your Friends

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi -Zanzibar

 Maafisa wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama hapa nchini pamoja na Mamkala ya Bandari Zanzibar, wamefanya oparesheni maalum ya ukaguzi wa meli ya AZAM Sealink -1 iliyoingia nchini juzi kuangalia kama ina ubora na kukidhi vigezo vya usafirishaji wa abiria na mizigo majini yakiwemo magari.

Maafisa waliofanya ukaguzi huo ni kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Usalama wa taifa, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Mamlaka ya Usalama Bandarini na Huduma za Meli Zanzibar (ZMA) na Mamlaka ya Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA).

Pamoja na kuangalia ubora na vigezo vingine, Maafisa hao pia wamepata maelezo toshelezi juu ya ubora wa meli hiyo kutoka kwa Kampuni ya RFI iliyopewa dhamana ya kuisafirisha Meli hiyo kutoka nchini Ugiriki hadi hapa nchini.

Akizungumza na Ujumbe huo ndani ya Meli hiyo iliyoweka nanga nje kidogo ya Bandari ya Zanzibar, Mkurugenzi wa RFI Bw. Stefan Nedkoff, alisema kuwa meli hiyo imeweza kusafiri yenyewe kutoka nchini Ubeligiji hadi hapa nchini pasipo msaada wowote wa kiufundi.

Amesema kuwa katika maeneo waliyopitia walipambana na kila aina ya dharuba na kuvuka vikwazo vya mikondo mikubwa ya bahari kwenye kina kirefu na Meli hiyo iliweza kuhimili hali hiyo.

Alisema Meli hiyo inayoongozwa kwa mifumo ya kompyuta, ina uwezo mkubwa wa kuhimili misukosuko ya hali ya bahari na kusafiri umbali na kina kirefu cha maji baharini pasipo shaka.

Bw. Nedkoff amesema kuwa, mbali ya kuwa meli hiyo ilisafiri ikiwa tupu, lakini itahimili vishindo zaidi vya baharini pale itakapokuwa na abiria na mizigo ya kutosha.

Amesema kuwa mbali ya uwezo wake wa kubeba abiria 1,500, lakini pia meli hiyo inauwezo wa kuchukua mizigo yakiwemo magari 200 kutoka eneo moja kwenda jingine vyote vikiwa na uzito wa tani 500 bila ya kuwa na tatizo lolote la kiusalama.

Maafisa walioitembelea meli hiyo, wameonyeshwa njia maalum za kujiokolea pamoja na vifaa muhimu vya kiusalama vinavyoweza kutumika kwa uokozi wakati itokeapo ajali majini.

Meli hiyo pia ina vitanda vya kutosha kwa ajili ya wagonjwa na abiria watakaojisikia kupumzika wakati wanapokuwa safarini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Zanzibar mara baada ya kuwasili kwa Meli hiyo, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Coastal Ferry inayomiliki Boti ziendazo kasi za Kilimanjaro, Bw. Hussein Mohammed Saidi, alisema meli hiyo itafanya safari zake kati ya Dar es Salaam, Zanzibar na Pemba.

Amesema Kampuni yake ambayo ipo kihuduma zaidi, pia itaangalia uwezekano wa kuweka viwango vya nauli itakayomfanya kila mtu kusafiri yeye pamoja na jamaa ama watoto wake bila ya kujinyima.

Bw. Hussein alisema watoto wenye umri wa kuanzia saa moja hadi mika mitano watasafirishwa bure na wanafunzi watatozwa nusu ya nauli ya mtu mzima kwa kila safari.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Web Directories
PageHeat