Tweeted this
Like this, be the first of your Friends
Ndege za Misri leo zimeshambulia kwa mabomu karibu na mpaka na Israel. Aidha imeripotiwa kuwa ndege hizo zimeendesha mashambulizi ya angani kuzunguka mji wa Sheikh Zuwaid, 10km kutoka Palestina, Ukanda wa Gaza, kufuatiwa na mapigano mara moja kati ya watu wenye silaha na vikosi vya usalama katika vituo vya ukaguzi kadhaa kaskazini mwa Sinai.
Misri imetumia vikosi na vifaru vya kivita jana Jumatano asubuhi, na mashahidi katika Sheikh Zuwaid wamesikika wakisema yakuwa walisikia milipuko baada ya ndege mbili za kijeshi zikaruka juu ya eneo hilo.
Watu karibu na mji huo walisema waliona magari matatu yakilipuliwa. Uongozi wa kijeshi umetoa taarifa kuwa walikuwa wameanza kurejesha utulivu katika Sinai. Askari waliingia al-Toumah kijijini, km 20 upande wa kusini, kufuatia taarifa kuwa wapiganaji walijificha huko. Aidha pia kuna taarifa kuwa wanamgambo 20 waliuawa. Habari na Reuters
August 9, 2012
MAJESHI YA MISRI YAENDESHA MAPIGANO DHIDI YA WANAMGAMBO WA SINAI
Millionfortune.com
KIMATAIFA
Facebook Blogger Plugin by JustNaira.com | Get Widget
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako hapa!